Airtel yashirikiana na UNESCO kuanzisha Radio za jamii Nchini - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Airtel yashirikiana na UNESCO kuanzisha Radio za jamii Nchini

Afisa mradi wa habari na mawasiliano UNESCO   Yusuph Al Amin akikabithi radio ya solar kwa mkazi wa kijiji cha Ololosokwan  wakati wa ziara ya kutembelea mradi wa Radio jamii ulioanzishwa chini ya udhamini wa Airtel kwa kushirikia na UNESCO,  Radio zaid ya 200 zilikabithiwa kwa wakazi wa kijiji hapo,  uzinduzi wa  Radio hii utafanyika  mwishoni mwa mwenzi juni,
 Afisa mradi wa habari na mawasiliano UNESCO   Yusuph Al Amin akionyesha jinsi gani radio ya solar inavyofanya kazi mara baada ya kukabithi Radio 200 kwa wakazi wa kijiji cha Ololoskwan wakati wa  ziara ya kutembelea mradi wa Radio jamii ulioanzishwa chini ya udhamini wa Airtel kwa kushirikia na UNESCO, Ololosokwani Radio  inategemea kuzinduliwa mwishoni mwa mwenzi juni, wakishuhudia kushoto ni mwakilishi wa Airtel Ahmed Juma katika ni Yannick Ndoinyo Mkurugenzi mtendaji IrkiRamat Foundation (RAMAT
 wafanyakazi wa Airtel Dua Kazimoto na Mercy Nyange wakiwa katika picha na wanawake wafanyabiashara wa vikundi vidogovidongo wa kijiji cha Ololosokwani wakati wakati walipotembela mradi wa radio unotegemea kuzinduliwa mwishoni mwa mwenzi Juni
wanakijiji cha Ololoskwan na wawakilishi wa UNESCO na Airtel wakiwa katika picha ya pamoja wakati walipotembela mradi wa radio unotegemea kuzinduliwa mwishoni mwa mwenzi Juni
XXXXXXXXX

Airtel yashirikiana na UNESCO kuanzisha Radio za jamii Nchini

*         Mikoa zaidi ya 10 nchini  kufikishiwa Radio za jamii

*         Lengo ni kukuza sekta ya mawasiliano  hususani  maeneo
yaliyo na chagamoto za kijamii.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na UNESCOwamejiunga kuendeleza sekta ya mawasiliano nchini na kuhakikishahuduma za mawasiliano ya radio zinawafikia wananchi wengi hasa walewanaoishi kwenye maeneo ya vijiji  zinavyokumbwa na  changamotonyingi za kijamii pamoja  na kukosekana kwa huduma za radio.

Airtel na UNESCO kwa kutambua umuhimu wa mawasiliano katika karne hiiya 21 na katika kuhakikisha jamii inapata habari za uchumi, siasa naza kijamii ambazo ndizo nyenzo muhimu kwa maendeleo ya jamii yeyoteduniani wameonelea ni vyema kwa kushirikiana na jamii husika kuanzisharadio za jamii (community Radios) ili kutoa nafasi kwa wananchi kupataelimu mbalimbali kwa kupitia Radio hizi zitakazoenea nchini kote.

Lengo kubwa la kuanzisha radio hizo ni kwasababu maeneo mengi yamekosahuduma hizi muhimu za mawasilino na hivyo kujikuta kuwa kwenye mifumoduni  ya kijamii  kama vile ukiketwaji wa wanawake, elimu duni, imani
za kishirikina, Umaskini , unyanyasaji wa kijinsia, kuenea kwa kasikwa ugonjwa wa ukimwi na matatizo mengine mengi.

Akiongea wakati walipotembelea Radio iliyopo Ololosokwani msimamizi wamradi na Afisa uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde alisema, "Airteltunajisikia furaha kuwafikia wananchi na wateja wetu kwa kupitiamtandao wetu uliompana zaidi, tunaamini kwa kupitia radio hizi elimu itatolewa kwa jamii, upatikanaji wa  habari za kiuchumi na biashara kutawezesha kuboresha shughulili za kiuchumi katika maeneo husika na nchi kwa ujumla,  pia radio hizi zitawapa wakazi kufahamu hali ya kisiasa nchini na kupata habari mbalimbali za ndani na nje ya nchi tofauti na ilivyo sasa.

Airtel tunawajali sana na ndio maana ndio mtandao pekee unaopatikanahapa kijijini  Ololosokwani , na leo hii pia bado tumepiga hatuanyingine kwa kushirikiana na wenzetu wa UNESCO kufikisha huduma yaradio pekee ya Tanzania kijinini hapa ambayo masafa yake yatasikikahadi vijiji vya jirani"

Airtel tunaendelea kutimiza dhamira yetu kwa kushirikiana na serikaliya jamuhuri ya muungano chini ya wizara husika kuhakikisha tunachangiakatika kufikisha huduma hii muhimu kwa watanzania na kuleta mabadilikoya kiuchumi na kijamiii katika maeneo yanayoonekana ni duni na ambayohayajafikiwa.

Naye Afisa mradi wa habari na mawasiliano UNESCO   Yusuph Al Aminalisema" mradi wa radio hapa kijiji cha Ololosokwani utawawezeshawakazi wa hapa kupata mawasiliano ya karibu na sehemu mbalimbali zaTanzania, kutawawezesha kujifunza mambo mapya, kutangaza mila nadesturi za kimasai, kuweza kufahama mambo ya utawala bora na kuwezakuhoji viongozi wao, kupata habari mbalimbali, na pia kuelimishawamasai kuendeleza tamaduni zao na maendeleo kwa ujumla.

"Tunawashukuru wenzetu wa Airtel kwa kushirikiana nasi katikakuuanzisha mradi huu kwa kupitia radio hii tutaweza kufikia vijiji 14pindi tutakapoanza kurusha matangazo"alisema Bw, Al AminBw Al-Amin pia aliongeza kwa kusema "Pamoja na mradi wa radio piatumeweza kuanzisha multimedia center itakayowasaidi wakazi wa kijijinihapa na shule ya sekondari iliyopokaribu kuweza kutembelea tovutimbalimbali na kuweza kupata huduma za internet"

Vile vile tumeanzisha mradi wa kuboresha nyumba zakimasai kuondoa moshi na kuongeza mwanga na tutajenga nyumba mbili za mfano hivyo tunategemea wakazi wa hapa watajenga nyumba za makazi zilizo na kiwango kulinganisha na sasa na mradi mwengine ni wa kuboresha maziwa ya ngome na nyama na kuweza kutengeneza viwanda vidogo na kutengeneza jibini na mwisho tunaanzisha mradi wa solar utakao wawezesha wakazi wahapa kupata um eme" aliongeza Al Amin.

Miradi yote hii imeanzishwa baada ya kuanza mradi wa radio na kuona maeneo mengine ambayo tunaweza kuyaboresha na kuleta mabadiliko kwa wakazi wa hapa alimalizia kwa kusema Bw, Al Amin

Akiongea na waandishi wa habari  mkazi wa kijiji cha ololoskwanialiyejitambulisha kwa jina la bi Nekisho Ndoinyo alisema hapa kijijini kwetu hatuna radio ya Tanzania tuaamini kabisa kwa kuanzishwa radio hii kutaleta mafanikio makubwa kwa vikundi vya kina mama na wakazi wa hapa kutangaza biashara zao, tutaweza kupata taarifa mbalimbali , tutaweza kutangaza mila yetu ya kimasai, watoto wetu watapata elimu na kuweza kujua nafasi mbalimbali za shule na kazi, hivyo basi nachukua fulsa hii kuwahamasisha wanakijiji kushiriki katika vipindi vya radio pale itakapoanza kurusha matangazo yake, tumefurahi sana kuweza kupata mawasiliano haya ya radio na tunashukuru sana Airtel na UNESCO kwa jitihada hizi.

Kwa upande wake mkazi wa kijiji cha ololosokwani bi Kootu Tome aliongeza kwa kusema tatizo kubwa la kijiji hicho ni mgogoro wa Ardhi na wawekezaji kuvamia maeneo yao hivyo naamini radio itatoa mwanga kwa jamii na kuweza kutambua haki yao ya kimsingi.

Mradi huu wa Radio za jamiii unaosimamiwa na UNESCO kwa kushirikiana na Airtel  unategemea kufunguliwa rasmi mwishoni mwa mwenzi Juni kwa kuzindua kituo cha Radio kilichopo Ololosokwani  Arusha. Mikoa mingine itakayofikishiwa radio za kujamii ni pamoja na  Kyela Mbeya, Uvinza Kigoma, Pemba na maeneo mengi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages