WASHINDI WA KWANZA WA JENERATA NA BAJAJ PROMOSHENI YA "VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO" WAPATIKANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WASHINDI WA KWANZA WA JENERATA NA BAJAJ PROMOSHENI YA "VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO" WAPATIKANA


 Meneja wa Bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza washindi wa Promosheni Vumbua Hazina chini ya Kizibo inayoendesha na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia zake za Tusker Lager, Plisner Lager na Serengeti Lager, kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda.


Meneja wa Bia ya Serengeti Premium Lager Allan Chonjo akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza washindi wa Promosheni Vumbua Hazina chini ya Kizibo inayoendesha na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia zake za Tusker Lager, Plisner Lager na Serengeti Lager, kutoka kulia ni Meneja wa bia ya Tusker Ritah Mchaki, Mrisho kutoka shirika la Bahati Nasibu ya Taifa na  Teddy Mapunda mkurugenzi wa Mawasiliano (SBL)


Droo ya kwanza kabisa ya promosheni inayoendelea ya kampuni ya bia ya Serengeti Breweries LTD (SBL) inayojulikana kama‘Vumbua hazina chini ya kizibo’ imefanyika leo katika ofisi za kampuni hiyo, maeneo ya Oysterbay jijini Dar Es salaam.



Kampuni ya bia ya Serengeti ni kampuni tanzu ya kampuni ya DIAGEO PLC (UK) ya Uingereza na kupitia bidhaa zake, Serengeti Premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni hii tangu wiki iliyopita. Promosheni hii ya aina yake iliyosheheni zawadi mbalimbali kubwa na ndogo kama vile Jenereta , Pikipiki , Bajaji , Gari na zawadi zingine nyingi zikiwemo pesa taslimu na bia za bure.





Droo hii leo, ilihudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya kampuni hii, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH MOBILE na wahakiki na wakaguzi kutoka PriceWaterHouseCoopers (PwC) kuonesha jinsi washindi wote watapatikana kihalali.





Akiongea katika hafla hii, meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager, Bw. Allan Chonjo amesema kwamba “Tayari tumeweza kupata washindi waliopata pesa taslimu na wakafanikiwa kupata pesa zao kupitia MPESA ndani ya masaa 24.  Pia, washindi wamepatikana ambao wamejishindia zawadi za vinywaji vilivyopo katika promosheni hii.  Naomba nisisitize, kwamba promosheni hii inalenga kuinua na kubadilisha maisha ya watanzania hususani wateja wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni yetu ikiwa ni sera mojawapo ya kampuni hii kuisaidia jamii kwa njia mbalimbali kupitia bidhaa zake zenye ubora wa kipekee.  Pia ningetaka niseme ni njia ya pekee ya kuwashukuru watanzania kwa ushirikiano wao kwetu”.





Mshindi wetu wa droo ya kwanza ni John Gati mwenye umri wa miaka thelathini na mbili kutoka Musoma ambaye amejishindia jenereta  pamoja na Godfrey Shao mwenye umri wa miaka ishirini na nne kutoka Mwanza aliyejinyakulia Bajaj.  Baada ya kuchezeshwa droo kwa umakini kabisa na Rita Mchaki -Meneja wa bia ya Tusker Lager alipiga simu kwa washindi  na ilikuwa dhahiri kwamba washindi walishtuka na kufurahia ushindi wao.  Baada ya maongezi machache, waliweza kujieleza vizuri majina yao kamili na wanapopatikana ili waweze kupatikana siku chache zijazo kwenye hafla fupi ya kuwakabidhi zawadi zao.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages