Miss Tabata kufanyika Juni 1 Dar West - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Miss Tabata kufanyika Juni 1 Dar West

Na Mwandishi Wetu 
 
Shindano la kumsaka mrembo wa Tabata, Miss Tabata 2012, litafanyika Juni 1 katika ukumbi wa Da West Park, Tabata.
 
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema kuwa onyesho hilo pia kutakuwa na sherehe kabambe ya kusherehekea miaka 10 ya Miss Tabata.
 
“Shindano la mwaka huu litakuwa ni la aina yake kwa sasabu hii itakuwa ni mwaka wetu wa 10 kuanda Miss Tabata. Tutakuwa na burudani nyingi kutoka nje na ndani ya nchi. Pia tutahakikisha tunashirikisha warembo bomba wenye hadhi ya kushinda taji la Miss World,” Kapinga alisema mratibu huyo wa Bob Entertainment na Keen Arts.
 
Kapinga alisema kuwa warembo waliyowahi kushinda mataji tofauti tofauti la shindano hilo pia watakuepo kusherekea miaka 10 ya Miss Tabata.
 
Warembo watakaoshiriki kwenye shindano wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Dar West Park.
Warembo hao ni Neema Saleh (18), Noella Michael (19), Queen Issa (20), Hycalisa Joseph (18), Phillios Lemi (19), Wikllihemina Mvungi (20) na Nightness Rajab (19). Wengine ni Suzanne Pancras (19), Caroline David (21), Khadija Nurdin (19), Jamila Omary (18), Advent  Mamkwe (21), Nadya Marjeby (21), Axer Peter (20), Rahama Hassan (19), Mercy Mlay (21) na Diana Simon Laizer (20).
 
Kapinga aliwaomba warembo wenye sifa kuendelea kujitokeza waweze kupata wawakilishi bora katika shindano la Kanda ya Ilala.
 
"Bado milango iko wazi, mrembo yoyote anayejiamini kwamba ana vigezo anakaribishwa. Tunataka shindano la mwaka huu liwe na ushindani zaidi,” mratibu huyo aliongeza.Warembo 10 watachaguliwa kushiriki mashindano ya Miss Ilala na baadaye Miss Tanzania.Mrembo anayeshikilia taji la Tabata ni  Faiza Ally.

Warembo wa Tabata wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano ya Miss Tanzania ambapo mwaka juzi Consolata Lukosi alishinda nafasi ya tatu kabla ya kutangazwa kuwa balozi wa kinywaji cha Redds. Katika shindano la mwaka juzi Julliet William pia alishinda nafasi ya tatu katika ngazi hiyo ya taifa.
 
Juliet ndiye anayeshikilia taji la dunia la Miss Progressive International.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages