Mbunge wa jimbo la Segerea (CCM) na naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe.
Makongoro Mahanga akilakiwa na wafuasi wa wake baada ya kuibuka kidedea
katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo iliyokuwa
inamkabili katika mahakama kuu ya Tanzania dhidi ya mgombea wa chama cha
Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bw. Fredi Mpendazoe.
Baadhi ya wafuasi wa Fredi mpendazoe na wafuasi wa Makongoro Mahanga wakiwa nje ya mahakama mara baada ya hukumu ya kesi hiyo kutolewa.
Wafuasi wa Freddy Mpendazoe wakiwa na picha ya aliyekuwa mgombea wao baada ya kushindwa kesi hiyo.
Askari wa jeshi la polisi wakiwa makini kulinda usalama mara baada ya kesi hiyo kuamuliwa katika mahakama kuu leo.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)