Meneja wa kinywaji cha Serengeti Premium Lager Bw. Allan Chonjo
akizungumza wakati wa kutangaza washindi wa Genereta na Bajaj katika
bahati nasibu ya promosheni ya Vumbua Hazina chini ya Kizibo
iliyofanyika kwenye ofisi za Kampuni hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam
kulia ni Tumainiel Malisa kutoka PWC.
Menejwa mawasiliano wa kampun i ya bia ya Serengeti Imani Lwinga
akizungumza wakati wa kuchezesha bahati nasibu hiyo katikati ni Meneja
wa bia ya bia ya Serengeti Premium Lager na kulia ni Tumainiel Malisa
kutoka PWC
Meneja wa kinywaji cha Serengeti Premium Lager Bw. Allan Chonjo
akizungumza wakati wa kutangaza washindi wa Genereta na Bajaj katika
bahati nasibu ya promosheni ya Vumbua Hazina chini ya Kizibo
iliyofanyika kwenye ofisi za Kampuni hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam
katikati ni Tumainiel Malisa kutoka PWC na kulia ni Abdallah Hemed
kutoka bodi ya mchezo ya kubahatisha.
Zoezi la kukabidhi zawadi kwa washindi
waliojitokeza kushiriki na kushinda zawadi zinazotolewa katika
promosheni ya kipekee ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’ inayoendeshwa na
kampuni ya bia ya Serengeti limeendelea wiki iliyopita katika mikoa ya
Iringa na Mwanza ambapo mshindi wa jenereta na yule
wa bajaj walikabidhiwa zawadi zao katika sherehe zilizohudhuriwa na
umati mkubwa wa watu na kushuhudia SBL ikikabidhi zawadi hizo na kuamsha
hamasa kubwa kwa wapenzi na watumiaji wa biadhaa za SBL.
Asubuhi ya leo droo ya tano ya
promosheni hiyo ‘VUMBUA
HAZINA CHINI YA KIZIBO’ imechezeshwa katika ofisi za kampuni ya bia ya
Serengeti zilizopo maeneo ya Oysterbay jijini na kupata kuhudhuriwa na
waandishi wa habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania,
wadau kutoka ndani na nje ya kampuni hiyo, wakiwemo kampuni ya kuendesha
Bahati Nasibu ya PUSH MOBILE na wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price
Water House Coopers.
Akiongea
katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa kuchezeshwa kwa droo ya
tano ya promosheni hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo bw.
Ephraim Mafuru, amesema “Tumeshakabidhi
jereta nne kwa washindi mbalimbali na zawadi ya pikipiki, bajaj mbili
na gari moja aina ya FORD FIGO ambapo zawadi zote zimeshakabidhiwa kwa
washindi wetu . Hivi karibuni tutasafiri kwenda Mfinga Mkoani Iringa
kukabidhi Bajaj”.
“Naendelea kuwashauri jamii na
watanzania kwa ujumla kwamba promosheni hii ni kwa ajili ya kila
mtanzania mwenye vigezo vya kushiriki kwa hiyo wajitokeze k kwa wingi
kushiriki ili kujaribu bahati kama wenzetu ambao wamejaribu na kupata
zawadi kubwa ambazo hawakutarajia katika maisha yao.” Alisema Mafuru.
Aliongeza kuwa zawadi zinazoshindaniwa
gharama yake ni jumla fedha za kitanzania milioni 780 ikiwemo pesa
taslimu ambazo mshindi anapata papo hapo kupitia matandao wa simu za
mikononi M- pesa. Ikumbukwe kuwa zawadi hizi zinapelekwa hadi pale
mshindi wetu alipo bila yeye kuchangia chochote walakugharamia chochote
ikiwemo usafiri.
Katika droo hii ya tano mshindi ni Isaya
Charles kutoka Igoma mkoani Mwanza ambaye amejishindia Jenereta, wakati
mshindi mwingine Mariam Karumba mwanafunzi wa mwaka wa tatu Chuo Kikuu
cha Saint Agustin pia anatoka mkoani Mwanza amejishindia Bajaj
Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia
bidhaa yake bora kabisa ya Serengeti Premium Lager, Tusker Lager and
Pilsner inaendesha promosheni hii kwa wiki 16 ikiwa na lengo la kuinua
na kuboresha maisha ya wateja wake na watanzania kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)