Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel imeongeza muda kwa wateja wake kuendelea kucheza promosheni yake
kabambe ya Nani mkali ambayo ilianza miezi mitatu iliyopita na
kuwafaidisha zaidi ya wateja 90 wa Airtel waliojishindia jumla ya
miliono 217 kwa mgawanyo wa kuanzia milioni 1 kila siku, milioni 3 kila
wiki na milioni 30 kwa washindi wa mwezi
Akiongea na waandishi wa habari leo Meneja
uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema promosheni hii
imekuwa na faida kwetu Airtel wateja wetu waliokuwa wakishiriki
wameifurahia na ndio maana leo tumeamua kuongeza zawadi na muda wa
promosheni ya Nani Mkali
Hivyo promosheni yetu inaongezwa muda wa
miezi miwili huku zawadi zitakazo toka ni pesa taslim Jumla ya ya
shilingi milioni 143 katika mgawanyo wa kuanzia shilingi milioni 1 kila
siku-washindi 52, milioni 3 kila wiki –washindi 7,na milioni 30 kwa
kila mwezi itatoka kwa washindi 2.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)