Hoja ya Zitto ya kutaka Waziri Mkuu Pinda apigiwe Kura ya Kutokuwa na Imani naye yakwama kutokana na kanuni za Bunge - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Hoja ya Zitto ya kutaka Waziri Mkuu Pinda apigiwe Kura ya Kutokuwa na Imani naye yakwama kutokana na kanuni za Bunge

Spika wa Bunge, Anne Makinda
Na Mwandishi Wetu-Dodoma

Spika wa Bunge, Anne Makinda amesema hoja ya kutaka kumpigia kura ya kutokuwa na imani Waziri Mkuu Mizengo Pinda, inayokusudiwa kupelekwa bungeni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), ni batili na haina nguvu kwa kuwa haijakidhi matakwa ya kanuni.

Amewataka wabunge kuzisoma kikamilifu kanunzi zinazohusiana na hoja hiyo.
 
Wakati Spika Anna akieleza hivyo, wabunge nao wamesema wana imani na utendaji kazi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda na wasingepanda kumwondoa katika wadhifa huo, lakini tatizo kubwa ni mawaziri wake.

Pia, wamesema hoja ya kutaka kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye, inalenga kumshinikiza kuwawajibisha mawaziri wanaotuhumiwa kwa vitendo vya wizi na kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Wakijadili taarifa za Kamati za Hesabu za Mashirika ya Umma, Serikali za Mitaa na Serikali Kuu, wabunge waliwashutumu mawaziri kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao kiasi cha wengine kwenda mbali zaidi kwa kuwatuhumu kuwa mawaziri wengi ni wezi na kwamba, wamekuwa wakijali maslahi binafsi kuliko ya wananchi wanaowaongoza.

Mawaziri waliokuwa wakishutumiwa na kutakiwa kuachia ngazi ni Mustafa Mkullo (Fedha), Dk. Cyril Chami (Viwanda na Biashara), George Mkuchika (TAMISEMI), Omar Nundu (Uchukuzi), ambapo wabunge waliwataka kuachia ngazi.

Kutokana na tuhuma hizo, Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini-CHADEMA), alitoa pendekezo la kuwataka wabunge 70 kusaini ili kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu.

Habari zilizopatikana bungeni jana zimesema wabunge 62 kati 70 wanaotakiwa, wamesaini pendekezo hilo huku wanne wakitoka CCM na mbunge pekee wa UDP, John Cheyo ndiyo hajasaini.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana, Zitto na Deo Filikunjombe (Ludewa-CCM), ambao ndiyo wanaratibu shughuli hiyo, walisema tatizo kubwa la wabunge si Waziri Mkuu Pinda bali mawaziri wasio waaminifu.

Zitto alisema tayari kazi ya kukusanya saini inaendelea na wana imani hadi kufikia leo jioni wangekuwa wamekamilisha idadi ya 70 kama kanuni inavyosema.

Amesema wabunge wa vyama vyote wamesaini ispokuwa UDP na kwamba, uongozi wa CUF umetoa maelekezo maalumu kwa wabunge wake kusaini.

Alisema miongoni mwa wabunge waliosaini wanne wanatoka CCM na kwamba, hoja hiyo ni ya wabunge wote bila kujali itikadi za vyama na lengo ni kutengeneza Bunge la utendaji badala ya kulalamika.

Iwapo hoja hiyo itapitishwa na Bunge, Pinda atakuwa Waziri Mkuu wa kwanza kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye.

Zitto amesema kuwa wanatarajia kuwasilisha hoja hiyo kwa Spika wa Bunge, Jumatatu kwa ajili ya hatua zaidi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages