RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA MRADI WA MAJI PAWAGA, UMEGHARAMIWA NA KANISA LA ANGLICAN KWA ZAIDI YA BILIONI MBILI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

demo-image

RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA MRADI WA MAJI PAWAGA, UMEGHARAMIWA NA KANISA LA ANGLICAN KWA ZAIDI YA BILIONI MBILI

j20Rais Jakaya Kikwete akifungua maji ya bomba kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi wa maji katika kijiji cha Itunundu kata ya Pawaga Iringa uliogharimiwa na kanisa la Anglican Dayosisi ya Luaha Mkoani Iringa kwa zaidi shilingi bilioni mbili, Huku wakuu wa kanisal hilo wakishuhudia, kutoka kulia ni Askofu mstaafu wa Dayosisi ya Luaha Dornald Mtetemela, Martha Mgomi Mratibu wa mradi huo na Askofu Joseph Mgomi wa Daayosisi ya Luaha. FULLSHANGWE ilikuwepo katika msafara huo na kukuletea taswira mbalimbali za kuwasili kwa Mh. Rais Jakaya Kikwete pamoja na shughuli yake ya kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Itunundu kata ya Pawaga mkoani Iringa.
j21Rais Jakaya Kikwete akimpongeza mama Agnes Msavi mara baada ya kumtwisha ndoo ya maji kuashiria ukombozi kwa mwanamke kutokana na kukamilika kwa mradi huo.
j24Baadhi ya waandishi wa habari wakiripoti tukio hilo huko Pawaga Itunundu.
j17Rais Jakaya Kikwete akiwasili kijijini Itunundu Pawaga tayari kwa kuzindua mradi huo.
j16Vijana wa Kimasai wakicheza ngoa yao wakati wakimkaribisha Rais jakaya Kikwete kijijini hapo leo.
j15Warembo wa kimasia wakiwmlaki Rais Jakaya kikwete huku wakiwa wameshikilia bendera za taifa alipowasili katika kijiji cha Itunundu.
j13Umati wa wananchi ukimsubiri Rais Jakaya Kikwete katika kijiji cha Itunundu.
j10Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Kamanda wa vijana mkoani Iringa Salim "Sas" Abri mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli mjini Iringa.
j11Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na kada wa Chama cha Mapinduzi Venance Mwamoto.
j12Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Askofu wa Dayosisi ya Luaha Joseph Mgomi wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli mjini Iringa leo mchana, kushoto ni Askofu mstaafu wa Dayosisi ya Luaha Dornald Mtetemela.
j8Rais Jakaya Kikwete akiwatunza wasanii wa kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitumbuiza wakati alipowasili mjini Iringa leo.
j7Rais Jakaya Kikwete akiongozana na Mkuu wa mkoa wa Iringa Dk. Christine Ishengoma kushoto mara baada ya kuwasili mjini Iringa leo, kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Grayson Rwenge.
j6Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Evarist Mangalla katika uwanja wa ndege wa Nduli.Picha Kwa Hisani ya Full Shangwe

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Pages