Rais Jakaya Kikwete Ameteua Makatibu Tawala wa Mikoa Saba na Kufanya Uhamisho wa Wengine Watatu - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Rais Jakaya Kikwete Ameteua Makatibu Tawala wa Mikoa Saba na Kufanya Uhamisho wa Wengine Watatu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, leo, Jumatano, Machi 21, 2012 ameteua Makatibu Tawala wa Mikoa saba na kufanya uhamisho wa wengine watatu.Ifuatayo chini ni taarifa kamili iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y.Sefue ikitangaza uteuzi huo:-

A: MAKATIBU TAWALA WA MIKOA

(i) Dkt. Faisal Hassan Haji ISSA, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa KILIMANJARO. Kabla ya hapo Dkt. Faisal alikuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Rasilimali Watu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

(ii) Bibi Mariam Amri MTUNGUJA, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa MBEYA. Kabla ya hapo Bibi Mtunguja alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea.

(iii) Bwana Eliya Mtinangi NTANDU, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa MOROGORO. Kabla ya hapo Bwana Ntandu alikuwaKatibu Tawala Msaidizi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Dar es Salaam.

(iv) Bwana Severine Bimbona Marco KAHITWA, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa GEITA. Kabla ya hapo Bwana Kahitwa alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Uchambuzi wa Sera, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dodoma.

(v) Eng. Emmanuel N.M. KALOBELO, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa KATAVI. Kabla ya hapo Eng. Kalobelo alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmasharui ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi.

(vi) Bwana Hassan Mpapi BENDEYEKO, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa RUVUMA. Kabla ya hapo Bwana Bendeyeko alikuwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro.

(vii) Dkt. Anselem Herbert Shauri TARIMO, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa SHINYANGA. Kabla ya hapo Dkt. Tarimo alikuwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma.Uteuzi huu unaanzia tarehe 21 Machi, 2012. Wataapishwa Ikulu, Jumamosi tarehe 24 Machi, 2012 saa nne asubuhi.

B: UHAMISHO

(i) Bibi Mgeni BARUANI – Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro
anahamishiwa Mkoa wa NJOMBE.

(ii) Bibi Mwamvua A. JILUMBI – Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga
anahamishiwa Mkoa wa SIMIYU.

(iii) Bibi Bertha O. SWAI, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya anahamishiwa
Mkoa wa PWANI.

Balozi Ombeni Y. Sefue
KATIBU MKUU KIONGOZI
IKULU,

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages