Meneja wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Mbeya, Calvin
Martine akitoa maelezo kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya, kuhusu
uzalishaji wa bia walipotembelea kiwanda hicho, mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya waandishi wa habari wa jijini Mbeya wakitembelea kiwanda cha
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kilichopo Iyunga jijini humo mwishoni
mwa wiki.
Baadhi ya waandishi wa habari wa jijini Mbeya wakishindana kutambua ladha ya bia za kampuni ya Bia Tanzania (TBL)
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Habari Leo Joachim Nyambo akipokea
zawadi ya katoni ya Bia aina ya Ndovu kutoka kwa Meneja Uhusiano na
Mawasiliano Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi baada ya kuibuka
mshindi wa kubaini ladha halisi ya aina ya vileo vinavyotengenezwa na
kampuni ya Bia ya TBL.Mashindano hayo yaliyohusisha wannahabari wa mkoa
huo yalifanyika mwishoni mwa wiki.Picha Kwa Hisani Ya Full Shangwe





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)