Mke
Wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal,
akisalimiana na mmoja kati ya watoto Yatima, Juma, baada ya kuwasili
kwenye Kituo cha kulelea watoto Yatima cha Katandala kilichopo
Sumbawanga jana kwa ajili ya kukabidhi Tanki la kuhifadhia maji la Lita
5000 katika kituo hicho.
Mke
wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal,
akisalimiana na mfanyakazi wa kujitolea kutoka nchini Ujerumani, Liza
Gernemann, aliyembeba motto William wa Kituo cha kulelea Watoto Yatima
cha Katandala, wakati alipofika katika kituo hicho jana kwa ajili ya
kukabidhi Tanki la kuhifadhia maji la Lita 5000.
Mke
wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal,
akiwa amembea mmoja kati ya watoto Yatima wanaolelewa katika Kituo cha
kulelea watoto hao katika Kituo cha Katandala, wakati akitembelea katika
vyumba vya kulala vya watoto hao, alipofika kukabidhi Tanki la maji la
Lita 5000 kituoni hapo jana. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Sumbawanga na Katavi, Eng. Stella Manyanya.
Mke
wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal,
kishikana mkono na Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto Yatima cha
Katandala, Sr. Maria Goreth Chusu, ikiwa ni ishara ya kumkabidhi Tanki
la kuhifadhia maji la Lita 5000 katika kituo hicho alipofika kituoni
hapo kilichopo Sumbawanga jana. Kushoto kwa Mama Asha ni Mkuu wa Mkoa wa
Sumbawanga na Katavi, Eng. Stella Manyanya (kushoto) ni Sr. Scolastica
Mwembezi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)