


Benki ya
Taifa ya Biashara (NBC) leo imekabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi
bilioni moja kwa Kampuni mahususi ya Kutafuta Fedha na Kutoa Mikopo ya
Muda Mrefu ya Nyumba iitwayo Tanzania Mortgage Refinance Corporation
(TMRC) ikiwa ni kiasi cha kununua hisa za asilimia 10.87 kwenye
kampuni hiyo. TMRC ni taasisi ya kifedha inayomilikiwa na mabenki
mbali mbali kwa lengo la kusaidia mabenki yaweze kutoa mikopo ya muda
mrefu ya nyumba kwa wateja.
Lengo
kuu la TMRC ni kusaidia kutoa fedha kwenye soko la kifedha la
Tanzania kwa ufanisi, na kuzilenga fedha hizo kwa mabenki wanachama
kwa viwango vya ushindani. Hii itawezesha upatikanaji wa makazi kwa
watanzania, na pia kuchangia maendeleo ya masoko ya mitaji.
Shughuli
hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki ya NBC, ikiongozwa
na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bwana Lawrence Mafuru.
Akizungumza
kwenye tukio hilo, Bwana Mafuru alisema: “Tunaamini kuwa fedha hizi
zitaiaidia TMRC katika juhudi zake za kuwawezesha Watanzania wapate
kumiliki makazi bora. Kitendo hiki kinaonyesha dhamira ya NBC katika kusaidia sekta ya mikopo ya nyumba Tanzania ”
Hundi
hiyo imepokewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TMRC, Bwana Rished Bade
mbele ya viongozi wa ngazi ya juu wa kampuni hiyo pamoja na
wawakilishi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Mwezi
Oktoba 2011, NBC pamoja na benki nyingine sita zilisaini mkataba na
Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) kwa ajili ya kuwawezesha Watanzania
kipata makazi bora zaidi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)