Katibu mkuu
wa CHADEMA Dr Willbroad Slaa akihutubia mjini Igunga jana katika
uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo jimboni hapa.Dr Slaaa alisema CCM
hawana sababu ya kuchaguliwa kwa nafasi yoyote ile kwani kwa kipindi
cha miaka 50 imeshindwa kumkomboa Mtanzania katika lindi la
umaskini.Aliongeza kuseam kuwa CCM wanachokizinatia ni kutumia kila
mbinu ili kushinda chaguzi na kushika dola ikiwa hawana malengo na
mikakati madhubuti ya kumkomboa Mtanzania. Aliwaasa wana Igunga
kumchagua Mgombea wa Chadema, Joseph Kashindye, ili awe mwakilishi wao
kwani ni mtu makini anaetoka katika chama makini.
Mwenyekiti
wa CHADEMA,Freeman Mbowe akihutubia maelfu ya wana Igunga jana katika
mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chaguzi mdogo jimboni la igunga.Mbowe
alisema kuwa wana Igunga mungu amewapa bahati kubwa ya ufaya uchaguzi
muda ,fupi baada ya uchaguzi mkuu. Hivyo waitumie bahati hiyo wa
kufanya mabadiliko. CCM haistaili kurudishwa tena madarakani jimboi
hapa, kwani kuna masuala mengi ya msingi yanayohusiana na maendeleo ya
wananchi CC imeshindwa kuyatekeleza kwa kipindi cha miaka 50.
Ilifika zamu ya Mgombea wa Ubunge jimboni
hapa kwa Tiketi ya Chadema, Mwalimu, Mkaguzi wa Elimu, Joseph
Lashindye.Kashindye alisema kuwa wana Igunga wtarajie mabadiliko ya
haraka katika maendeleo.Yeye ameamua kwa makusudi kuacha ualimu na
kuingia katika ulingO wa siasa. Amefanya kama Mwalimu Nyerere
alivyofanya kwani Mwalimu Nyerere, aliaacha ualimu na kujiunga na TANU,
matokea ya uamuzi huo wa mwalimu hakuna Mtanzania asiyeyaju.Na yeye
alisema kuwa endapo wana-Igunga watamapa ridhaa ya kuwa mwakilishi
atasimamia kwa nguvu zake zote misingi ya utu, uchapakazi na
atahakikisha anaziba mianya yote ya rushwa katika halmashauri ya
wilaya, ili fedha zinazotafunwa na wajanja, zifanye kazi iliyokusudiwa
ya kuwaletea maendeleo wana- Igunga.
Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika
akiwahutubia wananchi wa jimbo la Igunga jana jioni katikauzinduzi wa
kampeni za ubunge jimboni humo.
Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini Mh. Joseph
Mbilinyi akiwahutumia wakazi wa Igunga.
Mwenyekiti
wa CHADEMA, Freeman Mbowe akihutubia maelfu ya wana Igunga jana katika
mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chaguzi mdogo jimboni la igunga.
Sehemu Kubwa
ya Umati wa Wanachama Wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo(Chadema)akielekea kwneye uzinduzi rasmi wa kampeni za Kuwania
jimbo hilo.
Picha na Mdau Victor Makinda na CHADEMA
Mabango yalikuwa ni mengi lakini pia jeshi la
polisi lilihakikisha kunakuwa na usalama wa kutosha.
Anaitwa Joseph Kashinye, Mgombea ubunge kwa
tiketi ya CHADEMA jimbo la Igunga. "Ninashughulikia kupata mtandao wa
uhakika. Leo siku haitoisha, nitakuwa nimepata suluhu la tatizo la
Mtandao. Nitawaporomoshea kila kinachojiri huku. Asubuhi hii
nimebahatisha kuingiza picha hiyo kwa taabu, imenichukua saa mbili
kuingiza picha moja! Pichani Kashindye alikuwa akihutubia maelfu ya
wakazi wa Igunga katika uzinduzi wa kampeni jana.
Mabango
yenye ujumbe tofauti katika mkutano wa CHADEMA jana.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)