Pages

UJUMBE WA MFUKO WA KIMATAIFA WA MAENDELEO YA KILIMO "IFAD" WATEMBELEA PROGRAMU YA KUENDELEZA KILIMO NA UVUVI "AFDP" TANZANIA

Ujumbe kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) ukiwa umeambatana na watumishi wa Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), kutoka  Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) pamoja na watekelezaji wa programu hiyo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, TAMISEMI na Wizara ya Uchumi wa Buluu na uvuvi Zanzibar na Sekretariet ya Mkoa wa Morogoro wakijadiliana jambo na wanakikundi cha UWASAMO tarehe 6/11/2024
Ujumbe wa Timu ya wataalam kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD),  Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Wizara ya Mifugo na Uvuvi, TAMISEMI, Wizara ya Uchumi wa Buluu na uvuvi Zanzibar wakijadiliana jambo na wanakikundi cha UWASAMO wakati walipotembelea baadhi ya mabwawa ya Kikundi cha UWASAMO yanayotumika kwa ajili ya ufugaji samaki aina ya SATO yaliyopo katika kijiji cha Kingo

Ujumbe kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) ukiwa umeambatana na watumishi wa Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), kutoka  Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) pamoja na watekelezaji wa programu hiyo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Wizara ya Uchumi wa Buluu na uvuvi Zanzibar  wamekitembelea Kikundi cha Ufugaji wa samaki kiitwacho UWASAMO, katika kata ya Mzinga Mtaa wa Konga Manispaa ya Morogoro, ili kuona mafanikio ya ufugajiwa samaki kwa wanakikundi baada ya kupata mafunzo ya Ufugaji samaki, biashara na utunzaji wa kumbukumbu kutoka  kituo cha Kingolwira.

Ziara hiyo imefanyika tarehe 6/11/2024 kwenye Kituo kinachojishughulisha na utoaji mafunzo ya ufugaji samaki, pamoja na uuzaji wa vifaranga vya samaki.

Akizungumza kwa niaba ya wanakikundi ndugu Asungushe Patrick Msugupakulya amesema, wao kama kikundi wanaishukuru serika kwa kuwaletea mradi wa IFAD, ambao umewasaidia katika kuunda ushirika wao ambao mpaka sasa wanaendelea kupata msaada wa Elimu ya ufugaji wa samaki kwa wakati.

Pamoja na hayo wanakikundi cha UWASAMO, wamefurahishwa na ziara ya viongozi, ambapo wanaamini kwa kutembelewa huko, misaada zaidi watapata ili kuendeleza mtaji wao wa ufugaji wa samaki na kuleta maendeleo yenye tija kwa familia na Tanzania kwa ujumla wake.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)