Pages

Premier Bet waja kivingine na Footbal Jackpot King na Cash Out

 Meneja rasilimali watu na utawala wa Kampuni ya Premier Bet Tanzania Amanda Kombe akizungumza kuhusiana na huduma Mpya mbili walizoleta Kwa Wateja wao wa Mtandaoni na wanaotumia mawakala zijulikanazo kama Football Jackpot King na Cash Out.
 Mmoja wa Mabalozi wa Premier Bet, Jacob Mbuya akizungumzia Huduma mpya ya Cash Out iliyoanzishwa na Kampuni ya Kubashiri ya Premier Bet mapema leo Ofisini kwao 
Mabalozi wa Premier Bet wakiwa pamoja na Wafanyakazi wa Premier Bet mara baada ya kumaliza kutambulisha huduma mpya mbili zijulikanazo kama Football Jackpot King na Cash Out.

Kampuni ya michezo ya kubashiri ya premier bet Tanzania leo imekuja kivingine kwa kuleta huduma nyingine mbili mpya ambazo ni Football Jackpot King na Cash out huku huduma ya Football Jackpot King itakuwa maalumu kwa wateja watakaobashiri kupitia tovuti tu huku mshindi akishinda mpaka Milioni 500 za Kitanzania na Huduma ya Cash Out ikiwa kwa watumiaji wanaotumia mawakala wa Premier Bet popote pale Nchini.

Premier Bet yaleta huduma ambayo ni ya kwanza kabisa nchini katika uwanja wa kubashiri ambapo huduma hio inampa nafasi mteja wa premier bet kurudisha pesa yake pale anapohisi moja ya mechi katika mkeka wake inaweza kumfanya asishinde. Huduma hii ni huduma ya kwanza kabisa nchini huku ikiwapa nafasi wateja kurudisha pesa zao.

Football Jackpot King hii hupatikana kwa wateja wanaotumia tovuti tu huku mteja akiweka timu 18 na endapo timu zote 18 atakazoweka na kupatia matokeo basi Mteja huyo ataibuka na kitita cha Shilingi Milioni 500 lakini pia wale wataoapatia kuanzia mechi 15 na kuendelea watapata kifuta jasho.

Premier Bet imekuwa kampuni ya kwanza Tanzania kuanzisha huduma hii ya Cash out na Football Jackpot King huku wateja wake wakinufaika zaidi na Premier Bet. 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)