Pages

Pigo tena Clouds, Ephraim Kibonde Afariki Dunia Alfajiri ya Leo Mwanza.

Ni siku tatu tu tokea aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa CLouds Bw Ruge Mutahaba Kuzikwa leo Clouds imepata pigo jingine la kuondokewa na Mtangazaji wa Kipindi cha Jahazi cha Ephraim Kibonde ambae amefariki dunia alfajiri ya leo tarehe 7 Machi 2019 katika Hospitali ya Bugando iliyopo Jijini Mwanza amabpo alikuwa akipatiwa matibabu baada ya Kuzidiwa na Presha wakati wa Kumzika aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Media Ruge Mutahaba ambaye alizikwa kijijini Kwao Kiziru Mkoani Kagera Jumatatu ya tarehe 4 Machi 2018.
Ephraim Kibonde alikua moja ya watangazaji (MC) katika Shughuli hio ya Msiba wa Aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Ruge Mutahaba.

Pamoja na Kuwa alikuwa mtangazaji wa Kipindi cha Jahazi na vipindi vingine vya television bado alikuwa akijihusisha na Maswala ya Ushereheshaji katika Shughuli mbalimbali lakini pia Alikuwa Mlezi wa Kundi la Waimbaji wa Tanzania la Weusi
Tunatoa Pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki
Mungu Ampumzishe Mahala Pema Peponi Amen

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)