Pages

NMB yatoa msaada wa Vitanda vya wagonjwa 9 katika Kituo cha Afya Kigamboni

DSC_1308
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (mwenye miwani kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitanda vya wagonjwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Bw. Ng'wilebuzu Lubigija vilivyotolewa kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Kigamboni jijini Dar es Salaam.


DSC_1177
Sehemu ya vitanda vilivyotolewa na Benki ya NMB kwa Kituo cha Afya cha Kigamboni jijini Dar es Salaam. Vitanda hivyo sita (6) vikiwa vya wagonjwa wa kawaida na vitatu (3) vikiwa maalum kwa ajili ya kujifungulia wajawazito vinathamani ya shilingi milioni tano.

DSC_1256
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (katikati) akizungumza leo kwenye hafla ya NMB kukabidhi msaada wa vitaanda vya wagonjwa kwenye Kituo cha Afya cha Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Bw. Ng'wilebuzu Lubigija na mgeni rasmi katika hafla hiyo.

DSC_1288
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Bw. Ng'wilebuzu Lubigija (kushoto) akizungumza leo kwenye hafla ya kupokea msaada wa vitanda vya wagonjwa kwenye Kituo cha Afya cha Kigamboni jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd akifuatilia.

DSC_1227
Diwani Kata ya Kigamboni, Mh. Dotto Msawa akizungumza leo kwenye hafla ya kupokea msaada wa vitanda vya wagonjwa kwenye Kituo cha Afya cha Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Bw. Lubigija wakifuatilia.

DSC_1201
Sehemu ya wafanyakazi wa kituo hicho pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.

DSC_1318
Picha ya pamoja ya wageni waalikwa mbele ya vitanda hivyo vilivyotolewa na Benki ya NMB.




Na Mwandishi Wetu

BENKI ya NMB imetoa msaada wa vitanda tisa vya wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Kigamboni jijini Dar es Salaam vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni tano.



Vitanda hivyo sita (6) vikiwa vya wagonjwa wa kawaida na vitatu (3) vikiwa maalum kwa ajili ya kujifungulia kwa wajawazito, vimekabidhiwa leo kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Bw. Ng'wilebuzu Lubigija.



Akikabidhi vitanda hivyo, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd alisema msaada huo ni sehemu ya utaratibu wa kawaida wa NMB kurejesha faida kidogo kwa jamii.



Alisema Benki hiyo, hutenga takribani shilingi bilioni moja kila mwaka ambayo hurejeshwa kwa jamii kwa kusaidia sekta za afya, elimu na masuala mengine yanayoikumba jamii kama maafa na majanga.



Alisema Benki ya NMB inaunga mkono juhudia za Serikali za kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo afya kwa wananchi, ili jamii ambao ni sehemu ya wateja wa benki hiyo wawe na afya njema.



"...Kama tunavyojua afya ni huduma ya msingi kwa jamii wakiwemo wateja wetu, hivyo tuna kila sababu ya kuisaidia pale tunapopata fursa ya kufanya hivyo," alisema Bw. Badru Idd katika hotuba yake.



Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Bw. Ng'wilebuzu Lubigija akipokea msaada huo aliipongeza Benki ya NMB kwa juhudi zake za kuendelea kusaaidia sekta mbalimbali za huduma za kijamii.



Naye Mganga Mfawidhi Kituo cha Afya Kigamboni, Dk. Julius Nyakazilibe alisema msaada wa NMB umefika wakati muafaka kwani kwa sasa kituo kinapanua huduma zake ikiwemo kuongeza majengo hivyo vitasaidia kuziba mapengo yanayojitokeza.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)