Pages

WAZIRI JENISTA MHAGAMA AZIAGIZA TAASISI ZA UMMA NA BINAFSI ZINAPOSAIDIA JAMII ZIKUMBUKE MAHITAJI YA MAKUNDI MAALUM


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (wapili kulia), Naibu Wake, Mhe. Stella Ikupa (wakwanza kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba (mwenye miwani), wakiangalia jinsi wanafunzi wasioona wanavyotumia mashine maalum za kuandika nukta nundu, kwenye chou cha walemavu Yombo jijini Dar es Salaam Septemba 17, 2018. Waziri Jenista amepokea mashine hizo maalum Braille Machines,  11 zilizotolewa na WCF ikiwa ni utekelezaji wa sera ya kusaidia jamii (CSR) ili zitumike kwanye taasisi za wanafunzi wasioona.
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, (pichani), ameziagiza taasisi za umma na binafsi nchini zinapotoa fedha za kusaidia jamii (CSR), zikumbuke kuna kundi maalum la walemavu nchini ambao nao wanahitaji huduma maalum kama wanavyohitaji wengine.

Mheshimiwa Waziri aliyasema hayo jioni ya Septemba 17, 2018 wakati akipokea mashine maalum za kuandika kwa wanafunzi wasioona (Braille Machines) kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwenye chuo cha walemavu Yombo jijini Dar es Salaam.

“Tunapoona kwenye shule za msingi wanahitaji madawati, tukumbuke kwamba, wapo wanafunzi kwenye vyuo,  wapo wanafunzi kwenye shule
za msingi, ambao ni wenye ulemavu ambao pengine badala ya madawati, wao wanahitaji viti vya kuwaongezea mwendo, au kama tunatoa computer mpakato, tukumbuke kwamba tunazo shule na vyuo watoto wetu, vijana wetu wanasoma wenye ulemavu wangehitaji mashine hizi zenye kuandika nukta nundu ili kuwasaidia wenye ulemavu ili na wao wafaidike na elimu katika nchi yetu ya Tanzania.”


Alisema Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama wakati akihutyubia kwenye hafla ya kukabidhi mashine hizo. Alisema, Amefarijika kuona maagizo ya Ofsii ya Waziri Mkuu, yameweza kutekelezwa na taasisi ambayo iko chini ya ofisi ya Waziri Mkuu, kwa kusaidia kundi hilo la
wenye ulemavu.

“Vifaa nitakavyovikabidhi leo ni maalum kwa wenzetu wasioona  na ni vya wanafunzi walioko katika vyuo mbalimbali kwenye nchi yetu siyo hapa Yombo peke yake.” Alifafanua.

Aliupongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa msaada huo mkubwa na kwamba fedha walizotumia kununua vifaa hivyo ni kuwekeza kwa vijana ili kujiandaa kuwa na utashi na weledi na kujiandaa kuingia kwenye soko la ajira nchini.

Akimkaribisha Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, ameitaka jamii ya watu wenye ulemavu nchini kujiamini, kujitambua, kujikubali na kutioa bidii katika kazi wanazofanya.

“Kama ni mwanafunzi weka bidii katika masomo, na kama ni mwajiriwa weka bidii katika kazi yako kwani huo ndio ukombozi kwa mtu mwenye ulemavu.” Aliasa Mhe. Ikupa. Alisema vifaa vilivyopokelewa ni muhimu sana kwa watu wenye ulemavu hususan kwa kundi la wasioona, kwani vitawawezesha katika dhama  nzima ya ujumuishwaji mtu mwenye ulemavu
anapopatiwa vifaa vinavyoweza kutekeleza majukumu yake anakuwa anawezeshwa kuwa katika ujumuishwaji kwa hiyo atajumuishwa katika elimu lakini hatimaye atajikuta amefikia kwenye eneo la ajira na hatimaye kujikomboa na kuon dokana na utegemezi na uombaomba.

“Nikiwa kama Naibu Waziri ninayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, nitoe pongezi za kipekee kwa uongozi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa tendo hili kubwa ambalo mmelifanya.” Alipongeza.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) Bw. Masha Mshomba alisema, Mwaka jana (2017) WCF ilifanya Mkutano wa kwanza wa mwaka na katika mkutano ule Mfuko uliahidi kupitia mpango wake wa kusaidia jamii (CSR) utasaidia watu wenye ulemavu na kwamba ahadi hiyo imetekelezwa.

“Tumetoa msada wa mashine hizi maalum (Braille Machines) 13 zenye thamani ya Shilinhgi Milioni 33.8 na tunaimani kwamba zitawasaidia sana wenzetu wasioona ili kuwafanya washiriki kwa ufanisi katika kujifunza.” Alisema.

Alisema, Sekta ya Hifadhi ya Jamii, WCF ikiwa ni miongoni mwa sekta hiyo, moja ya majukumu ambayo serikali inasisitiza ni kuhakikisha ushiriki wa sekta katika kuondoa changamoto kwenye makundi maalum na hatua hiyo ya kutoa msada ni utekelezaji wa maagizo hayo ya serikali.

Katika awamu hii ya kwanza taasisi zilizofaidika ni pamoja na Chuo cha Ufundi kwa Walemavu, Yombo na Sabasaba kilichoko Singida, Shule za Uhuru Mchanganyiko ya Dar es Salaam, Shule ya Msingi Ndanda, iliyoko Mkoani Mtwara, Shule ya msingi Biharamulo, Shule ya Msingi Mgeta Mseto Bukoba Mkoani Kagera. 
Mhe. Waziri Jenista Mhagama (kushoto), akiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Anayeshughulikia masuala ya wenye ulemavu), Mhe. Stella Ikupa, wakati akizungumza kwenye hafla hiyo.
 Mhe. Stella Ikupa, (Kulia), akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba
 Baadhi ya wanafunzi wanaosoma kwenye chou cha ufundi kwa watu wenye ulemavu Yombo jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye hafla ya kupokea msada wa mshine za kuandika nukta nundu (Braille Machines)
 Baadhi ya wanafunzi wanaosoma kwenye chou cha ufundi kwa watu wenye ulemavu Yombo jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye hafla ya kupokea msada wa mshine za kuandika nukta nundu (Braille Machines)
 Wanafunzi wakijadiliana wakati wa hafla ya kupokea msaada wa mashine za kuandika nuka nundu (Braille Machines) Septemba 17, 2018.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (anayeshuhulikia masuala ya Wenye ulemavu), Mhe. Stella Ikupa, akilakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF Bw. Masha Mshomba na viongozi wengine, wakati akiwasili kwenye hafla hiyo.
 Waziri Mhe. Jenista Mhagama, (katikati), akipokelewa na Kaimu Mkuu wa Chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu Yombo jijini Dar es Salaam, (Kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, wakati akiwasili chuoni hapo Septemba 17, 2018.
 Wanafunzi wakishangilia
 Bw. Mshomba akijadiliana na wasaidizi wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasilianona Uhusiano, Bi. Laura Kunenge, na Afisa Uhusoiano Mwandamizi, Bw. Fulgence Sebera.
 Waziri Mhagama, akimkabidhi mashine hiyo, Kaimu Mkuu wa Chuo cha ufundi kwa wanachuo walemavu Yombo, Bi. Mariam, wapili kushoto), huku Naibu Waziri Mhe. Stella Ikupa (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa WCF Bw. Masha Mshomba wakishuhudia.
  Waziri Mhagama, akimkabidhi mashine hiyo, Kaimu Mkuu wa Chuo cha ufundi kwa wanachuo walemavu Yombo, Bi. Mariam. Kushioto ni Bw. Masha Mshomba.
 Kaimu Mkuu wa chuo cha ufundi kwa walemavu Yombo, Bi. Mariam, (kushoto) akitoa neon la shukrani.
 Picha ya pamoja.
 Mmoja wa wanafunzi akionyesha kipaji cha kusakata muziki wa Bongo Flava
 Mhe. Jenista Mhagama, akikishajihisha kikundi cha kwaya ya 
 Mhe, Waziri akimkabidhi mbunge wa Ndanda Mhe. Cecil Mwambe.
Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi mashine mwakilishi kutoka Shule ya Uhuru Mchanganyiko ya Dar es Salaam, Bi.Mwilongo Mtamike.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)