Pages

Tanzania kuendelea kuhimiza maendeleo ya viwanda

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Tausi Kida (kushoto) akimuonyesha Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristide Mbwasi aliyemwakilisha Katibu Mkuu Viwanda wa Wizara hiyo Bw. Joseph Simbakalia Sera ya viwanda endelevu: Mchango wa mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na biashara mara baada ya kuwasili ofisi za ESRF kufungua mkutano wa sita wa kitaifa wa uragibishi (NRG6) wenye lengo la kufanya sera ya viwanda endelevu kwenda sanjari na mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula huku ikiimarisha uchakataji wa mazao ya kilimo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho ESRF, Profesa Fortunata Makene.
 Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristide Mbwasi akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba Katibu Mkuu Viwanda wa Wizara hiyo Bw. Joseph Simbakalia wakati wa mkutano wa sita wa kitaifa wa uragibishi (NRG6) wenye lengo la kufanya sera ya viwanda endelevu kwenda sanjari na mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula huku ikiimarisha uchakataji wa mazao ya kilimo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki na mgeni rasmi wakati wa mkutano wa sita wa kitaifa wa uragibishi (NRG6) wenye lengo la kufanya sera ya viwanda endelevu kwenda sanjari na mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula huku ikiimarisha uchakataji wa mazao ya kilimo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristide Mbwasi (katikati) aliyemwakilisha Katibu Mkuu Viwanda wa Wizara hiyo Bw. Joseph Simbakalia akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua Sera ya viwanda endelevu: Mchango wa mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na biashara wakati wa mkutano wa sita wa kitaifa wa uragibishi (NRG6) wenye lengo la kufanya sera ya viwanda endelevu kwenda sanjari na mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula huku ikiimarisha uchakataji wa mazao ya kilimo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Tausi Kida (wa pili kushoto), pamoja na waandishi wa Sera ya viwanda endelevu: Mchango wa mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na biashara,  Kutoka kushoto ni Dr. Deusdeit Rwehumbiza (kushoto), Profesa Samuel Wangwe (wa pili kulia) na John Shilinde (kulia).
 Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristide Mbwasi (katikati) aliyemwakilisha Katibu Mkuu Viwanda wa Wizara hiyo Bw. Joseph Simbakalia, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Tausi Kida (wa pili kushoto), pamoja na waandishi wa Sera ya viwanda endelevu: Mchango wa mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na biashara Dr. Deusdeit Rwehumbiza (kushoto), Profesa Samuel Wangwe (wa pili kulia) na John Shilinde (kulia) kwa pamoja wakionyesha nakala ya sera hiyo iliyochapishwa CUTS International kwa ufadhili wa serikali ya Sweden.
 Mtafiti mshiriki mwandamizi wa ESRF Prof Samuel Wangwe akiwasilisha mada kuhusu mambo yanayostahili kuwepo katika sera mpya ya viwanda endelevu – SIDP- kwenye mkutano wa sita wa kitaifa wa mashauriano  wakati wa mkutano wa sita wa kitaifa wa uragibishi (NRG6) wenye lengo la kufanya sera ya viwanda endelevu kwenda sanjari na mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula huku ikiimarisha uchakataji wa mazao ya kilimo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam
 Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki kutoka serikalini, taasisi za kitaifa, wafanyabiashara , taasisi zisizo za kiserikali, waandishi wa habari, wanazuoni wawakilishi wa wakulima, makundi ya wanawake na wawakilishi kutoka UNFCCC wakishiriki katika mkutano  wa sera mpya ya viwanda endelevu. wakichangia mada wakati wa mkutano wa sita wa kitaifa wa uragibishi (NRG6) wenye lengo la kufanya sera ya viwanda endelevu kwenda sanjari na mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula huku ikiimarisha uchakataji wa mazao ya kilimo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Tausi akichangia mada wakati wa mkutano wa sita wa kitaifa wa uragibishi (NRG6) wenye lengo la kufanya sera ya viwanda endelevu kwenda sanjari na mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula huku ikiimarisha uchakataji wa mazao ya kilimo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya washiriki kutoka washiriki kutoka serikalini, taasisi za kitaifa, wafanyabiashara , taasisi zisizo za kiserikali, waandishi wa habari, wanazuoni wawakilishi wa wakulima, makundi ya wanawake na wawakilishi kutoka UNFCCC wakishiriki katika mkutano wa sita wa kitaifa wa uragibishi (NRG6) wenye lengo la kufanya sera ya viwanda endelevu kwenda sanjari na mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula huku ikiimarisha uchakataji wa mazao ya kilimo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi wetu
SERIKALI ya Tanzania imesema kwamba itaendelea kuhimiza uwapo wa viwanda kila mkoa kama sehemu ya kuleta mabadiliko makubwa ya uchumi nchini kote.

Aidha imesema itaendelea kuhakikisha kwamba maendeleo hayo yanasaidiwa na sera ya viwanda endelevu kwa lengo la kuliwezesha taifa kuwa na kipato cha kati kwa kutegemea uchumi wa viwanda.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Joseph Simbakalia katika hotuba yake iliyosomwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Aristide Mbwasi wakati wa kongamano la sita kitaifa kwa ajili ya mradi wa PACT-EAC lililofanyika kwenye ukumbi ya Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo  wa wataalamu kutoka kada mbalimbali  nchini uliangalia uhusiano uliopo kati ya usindikaji wa bidhaa za kilimo, mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula pia  sera iliyopo.

Washiriki wa kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) walitoka katika taasisi za serikali, wafanyabiashara vyama visivyo vya kiserikali, wanahabari, wanazuoni wakulima na wajasiriamali wa bidhaa zinazotokana na kilimo.
Kwa mujibu wa Bw. Simbakalia kongamano hilo lilikuwa limelenga kuangalia hatua zilizofikiwa katika mchakato wa upitiaji Upya wa Sera ya Viwanda Endelevu (SIDP).

Mwezi Machi mwaka 2018 huu Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji ilijihusisha na kuangalia matokeo ya utafiti uliofanywa na ESRF kuhusu SIDP.

Kwa niaba ya serikali aliipongeza ESRF na CUTS international yenye makao makuu yake Geneva Uswiss kwa kuisaidia Wizara ya Viwanda kuiangalia upya SIDP ili kuwa na sera ambayo inazingatia mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula kwa kuangalia uchakataji wa mazao ya kilimo.

Sera Endelevu ya Maendeleo ya Viwanda (SIDP) (1996-2020) imeshatekelezwa katika hatua tatu ambapo ya kwanza ilianza 1996-2000 ikijikita zaidi katika ukarabati na uimarishaji wa uwezo wa viwanda vilivyokuwepo. Hatua ya pili (2000-2010) ilikuwa ni uzalishaji mpya wa uwezo kwa kuzingatia matumizi ya teknolojia na kujifunza; wakati awamu ya tatu (2010-2020) imelenga kufikia matokeo makubwa kwenye uwekezaji katika viwanda bidhaa mbalimbali na kuimarisha viwanda vilivyokuwapo na vilivyoundwa katika awamu zilizopita.

Bw. Simbakalia alisema kwamba kwa miaka mingi Sera Endelevu ya Maendeleo ya Viwanda (SIDP) imekuwa ikisaidiwa na sera kadhaa, mikakati na mipango mbalimbali ikiwamo mkakati wa maendeleo unaohusisha sekta mbalimbali ya mwaka 2025 na mpango wa maendeleo wa muda mrefu unaotekelezwa kwa hatua za miaka mitano mitano.

Mipango mingine ni kuimarisha kilimo, biashara na utumiaji wa taasisi za fedha kuendeleza ujasiriamali na kilimo.

“ Hakuna shaka kwamba harakati za kuwa na viwanda zimechanganywa vilivyo katika mipango ya maendeleo ya kitaifa. Hata hivyo athari za mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na biashara ya bidhaa za kilimo zilizochakatwa, zimekuwa hazihusishwi sana katika mipango hiyo ya maendeleo na utekelezaji wake” alisema Simbakalia.

Katibu huyo alisema anafahamu kwamba mkutano huo ni muhimu katika kuongeza vionjo vitakavyosaidia kuangalia upya sera ya sasa iliyopo ili kuifanya iendane na wakati huu ambapo kuna changamoto  kubwa katika mabadiliko ya tabia nchi.

Naye Mkurugenzi Mtedaji wa ESRF Dkt. Tausi Kida alisema wakati akimkaribisha mgeni rasmi kuhutubia alisema kwamba mkutano huo kuwa taasisi yake imepitia kwa ukamilifu SIDP kwa lengo la kuwawezesha watunga sera namna nzuri ya kuboresha sera iliyopo sasa ya viwanda endelevu.

Aliongeza  kwamba mkutano huo wa kitaifa wa sita wa mradi wenye lengo la kuboresha kilimo kwa kuangalia mabadiliko ya tabia nchi na biashara Afrika Mashariki (PACT EAC2), umeitishwa ili kuwapa wajumbe taarifa ya hali halisi ilivyo kwa sasa katika SIDP.

Alisema washiriki pia watapata nafasi ya kutaarifiwa hali halisi ilivyo sasa na majadiliano yanayoendelea huko WTO na UNFCC.

Alisema ni kweli kuwa kunahitajika mabadiliko katika SIDP ambayo tangu awali ilikuwa haielezei uhusiano uliopo kati ya kilimo, uchakataji mazao ya kilimo, usalama wa chakula na mabadiliko ya tabia nchi.

Mkurugenzi alisema pia mkutano huo ambao utawasaidia washiriki kutambua hatua iliyofikiwa na SIDP ili kuiwezesha kuwa na uhuishaji wa sera hizo na hali halisi ya sasa kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi.

Dkt. Kida alisema pamoja na upitiaji huo sekta binafsi imeonekana kuwa muhimu katika utekelezaji wa SIDP na kwamba mafanikio katika mchakato wake wa sasa unaweza kuambukizwa pia kwa Afrika Mashariki kupitia EAC Private Sector Development Strategy (PSDS) (2018 – 2022).

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)