Pages

NMB NA HALOTEL WASHIRIKIANA KUTOA KOMPYUTA NA INTANETI SHULE 200 ZA SERIKALI

IMG_9982

Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel Tanzania, Bw. Nguyen Van Son (wa pili kushoto) akipeana mkono na kubadilishaana nyaraka za makubaliano ya kiushirikiano na Mkurugenzi Mtendaji, Bi. Ineke Bussemaker (wa pili kulia) leo Dar es Salaam. Katika ushirikiano huo makampuni hayo yatatoa kompyuta kwa shule 200 za Serikali na kuziunganisha na huduma ya intaneti. 


IMG_9970

Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel Tanzania, Bw. Nguyen Van Son (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) wakisaini makubaliano ya kiushirikiano leo Dar es Salaam. Katika ushirikiano huo NMB na Halotel watatoa kompyuta kwa shule 200 za Serikali na kuziunganisha na huduma ya intaneti. 


IMG_9905

Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel Tanzania, Bw. Nguyen Van Son (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kwenye hafla hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji, Bi. Ineke Bussemaker pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda (kushoto) wakifuatilia.


IMG_9887

Mkurugenzi Mtendaji, Bi. Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel Tanzania, Bw. Nguyen Van Son pamoja na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd (kulia) wakishuhudia.


IMG_9955

 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Halotel, Mhina Semwenda (kushoto) akifafanua jambo katika hafla hiyo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji, Bi. Ineke Bussemaker na Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel Tanzania, Bw. Nguyen Van Son wakifuaatilia kwa makini.


IMG_0045

Mkurugenzi Mtendaji, Bi. Ineke Bussemaker na Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel Tanzania, Bw. Nguyen Van Son wakiangalia baadhi ya kompyuta ambazo zitatolewa katika ushirikiano huo.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

BENKI ya NMB pamoja na Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel nchini Tanzania leo zimesaini makubaliano yatakayozinufaisha zaidi ya shule 200 za Serikali kupata kompyuta na huduma ya intaneti bure ili zitumike kuboresha elimu kupitia teknolojia katika shule hiyo.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo jijini Dar es Salaam, ambapo Benki ya NMB imewakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji, Bi. Ineke Bussemaker na Kampuni ya Halotel imewakilishwa na Kaimu Mkurugenzi, Bw. Nguyen Van Son mbele ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali.

Akizungumza katika hafla hiyo, Bi. Bussemaker alisema NMB katika ushirikiano huo itatoa kompyuta zaidi ya 350 kwa shule 100 za Serikali huku Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel ikiziunganisha na huduma ya intaneti.

Alisema huduma hiyo ni endelevu ambapo kwa miaka mine iliyopita kompyuta 600 zilitolewa kwa shule mbalimbali na Halotel pia itaziunganisha na huduma ya intaneti. Kwa mwaka huu wa fedha takribani kumpyuta 400 zitatolewa nazo zitaunganishwa moja kwa moja na intaneti.

Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, Bw. Nguyen Van Son alisema hii si mara ya kwanza kwa kampuni yake kuunga mkono juhudi za Serikali kuboresha sekta ya elimu nchini. 

Akifafanua zaidi aliongeza kuwa Halotel imesaidia mipango kadhaa kuendeleza sekta ya elimu, ambapo ilitoa vifaa mbalimbali yakiwemo madawati shuleni, vitabu, mabegi, kujenga madarasa na kuweka vifaa vya kufundishia na kuziunganisha shule zaidi ya 417 na mtandao wa intaneti.

“Tofauti na mipango mingine kama hiyo, Halotel kwa ushirikiano na Kitivo cha CoICT cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) imeanzisha jukwaa la kujifunza linayoitwa Halostudy (http://www.halostudy.ac.tz) lenye maudhui ya Sayaansi na hisabati kwa masomo yote kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne inayofuata mtaala wa shule za sekondari za Tanzania,” alisema Bw. Nguyen Van Son.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)