Pages

BENKI YA NMB YAZINDUWA RASMI KLABU MAALUMU YA WAFANYABIASHARA TUNDUMA

Mkuu wa Wilaya ya Momba - Juma Irando akizungumza na wafanyabiashara wa Mkoa wa Songwe ambao ni wanachama wa NMB Business Club katika uzinduzi wa Business Club mpya uliofanyika mjini Tunduma juzi. Wengine kwenye picha ni Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu – Straton Chilongola (Kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Biashara cha NMB – Donatus Richard.
Mkuu wa Wilaya ya Momba - Juma Irando akikabidhi vyeti kwa wateja bora wa NMB Bank kwenye ufunguzi wa klabu mpya ya wafanyabiashara mkoani Songwe katika hafla iliyofanyika mjini Tunduma mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu – Straton Chilongola (Kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Biashara cha NMB – Donatus Richard.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara cha NMB – Donatus Richard (katikati) akizungumza kwenye uzinduzi wa Business Club mpya uliofanyika mjini Tunduma juzi.
Mkuu wa Wilaya ya Momba - Juma Irando akikabidhi vyeti kwa wateja bora wa NMB Bank kwenye ufunguzi wa klabu mpya ya wafanyabiashara mkoani Songwe katika hafla iliyofanyika mjini Tunduma mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu – Straton Chilongola (Kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Biashara cha NMB – Donatus Richard.
Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu – Straton Chilongola akizungumza kwenye uzinduzi wa Business Club mpya uliofanyika mjini Tunduma juzi.
Picha yapamoja kati ya mgeni rasmi paamoja na wakabidhiwa vyeti.

NA MWANDISHI WETU

BANKI ya NMB imezindua rasmi Klabu ya kibiashara maalumu kwa wafanyabiashara wa Tunduma katika wilaya ya Momba Mkoani Songwe. Kuzinduliwa kwa Klabu hiyo ya Biashara kunafanya klabu za biashara kuwa 35 nchini huku lengo lake likiwa ni kuwaunganisha wafanyabishara wa kati na wakubwa na kuwa chombo cha kutatua changamoto zinazo wakabili wafanyabiashara nchini.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Klabu ya Biashara mjini Tunduma juzi,  Mkuu wa Idara ya Biashara ya NMB – Donatus Richard alisema kuwa benki hiyo  imedhamiria kurahisisha huduma za kibenki kwa makundi mbalimbali hususani  wafanyabiashara ambao ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi nchini.

Bwana Donatus alisema kuwa ili kuhakikisha benki inachangia ukuaji wa sekta ya  biashara nchini, imeanzisha vilabu vya wafanyabiashara (NMB Business Clubs) ili  kukuza na kuimarisha biashara nchini.

Alisema kuwa NMB Business Club zina malengo ya kuifikia jamii ya 
wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa ambao wanajumuisha 
wafanyabiashara wateja wa NMB zaidi ya 50,000 nchi nzima huku biashara yao  ikifikia thamani ya shilingi bilioni 600. NMB Business Club ni mahali muafaka pa  kuelimisha wafanyabiashara juu ya masuala mbalimbali kuhusu biashara zao.

“Ndugu Mkuu wa Wilaya, Lengo la kuanzisha NMB Business Club ni kuhakikisha  wafanyabiashara hawa wanakuza mitaji yao, kuajiri watanzania wengi zaidi na pia  kuchangia uchumi wa taifa hili kupitia ulipaji kodi.” Alisema Donatus.

Donatus aliongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa NMB Busines Club, wanachama  wamekuwa wakinufaika na mafunzo mbalimbali ikiwemo jinsi ya kutumia vitabu vya mahesabu, elimu ya masoko na pia elimu ya mlipa kodi kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato nchini TRA.

Aidha katika hatua nyingine Donatus alisema Jumla ya Club 35 zime anzishwa na wanachama 20000 wameshanufaika na huduma zinazotolewa na NMB huku akieleza kuwa Mpango wa Bank ni kufikia wanachama 25000 ifikapo mwishoni  mwa mwaka 2018.

“Nmb Business Club zina malengo ya kuifikia jamii ya wafanyabiashara wadogo  na wa kati. Kwa sasa, Nmb Bank inahudumia wafanyabiashara zaidi ya 200,000 ambao ni wateja nchi nzima ambapo wana mikopo ya biashara yenye dhamni ya zaidi ya bilioni 600,” alisema Donatus.

Naye Mkuu wa Wilaya ya hiyo Juma Irando ambaye alikuwa mgeni rasimi kwenye hafla ya ufunguzi wa Busines Club alipongeza bank hiyo kwa kuamua kutoa elimu ya mlipakodi, utunzaji wa kumbukumbu na pia jinsi ya kuweka mahesabu sawa.

“Niipongeze Nmb kwa kutoa mafunzio haya kwani moja ya eno ambalo 
wafanyabiashara wengi wanakosa ni hili la Ulipaji kodi na utunzaji wa 
kumbukumbu hivyo niimani yangu kuwa litapunguza sana migogoro kati ya 
wafanyabisha na Serikali hasa TRA,” alisema Irando.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)