Pages

WAZIRI MKUU AIPONGEZA BENKI YA NMB KUCHANGIA HUDUMA ZA KIJAMII

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya sh. 10,000,000/= kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bibi Ineke Bussemaker (katikati) ukiwa ni mchango wa Benki hiyo kwa timu ya mpira wa miguu ya Namungo ya wilayani Rungwa. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam Mei 30, 2018. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa NMB, Bibi Vicky Bishubo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bibi Ineke Bussemaker (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa NMB (Head of Government Business), Bibi Vicky Bishubo, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Mei 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bibi Ineke Bussemaker (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa NMB (Head of Government Business), Bibi Vicky Bishubo, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Mei 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameipongeza Benki ya NMB kwa kuchangia huduma mbalimbali za kijamii zikiwemo elimu, afya na michezo.
Ametoa pongezi hizo leo (Jumatano, Mei 30, 2018) wakati akizungumza Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bi. Ineke Bussemaker ofisini kwake Magogoni jijini Dra es Salaam.
Amesema katika jitihada za Serikali za kufufua ushirika na hasa kwenye mazao makuu matano, wakulima wamehamasishwa wafungue akaunti ili malipo ya fedha zao yafanywe moja kwa moja kweye akaunti zao.
“Tumehamasisha wakulima wote wafungue akaunti ili malipo ya mazao yao yafanywe mojamoja katika akaunti zao jambo ambalo litaepusha wizi au kunyang’anywa fedha wawapo mitaani, na kupitia mawakala walioko vijijini, wataweza kupokea fedha hizo,” amesema.
Amesema uwepo wa mawakala wa benki hadi vijijini, umesaidia kuwafanya Watanzania wasiweke fedha ndani ya nyumba zao.
Akizungumzia mchango wa Benki hiyo kwenye huduma za jamii, Waziri Mkuu amesema benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kuchangia vitabu, madawati na michezo ambapo imetoa mchango wa sh.milioni kwa timu ya soka ya Namungo iliyoko wilayani Ruangwa.
“Tumeona Benki ya NMB ikifadhili timu mbalimbali za ligi kuu kama vile AZAM, na sasa wameanza kuchangia timu za daraja la kwanza kwa kuichangia timu ya Namungo shilingi milioni 10. Pia walichangia sh.milioni kwenye ujenzi wa uwanja wa kisasa kule Ruangwa, tunawashukuru sana,” amesema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Bussemaker alisema wamefurahi kupata fursa ya kuichangia timu ya Namungo na kwamba wataifuatilia kwa karibu kuona ushiriki wake ukoje kwenye ligi hiyo. “Pia tunaitakia kila la kheri kwenye ushiriki wao wa ligi daraja la kwanza,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)