Pages

Simba uso kwa uso na Gor mahia Sport pesa cup

Michuano ya Sportspesa

MABINGWA 
wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Timu ya Simba SC wamefanikiwa kutinga fainali za michuano ya Sportspesa Super Cup ya kampuni ya Sportspesa baada ya kuwacharaza timu ya Kakamega Homeboyz ya Kenya kwa mikwaju ya penati 5-4.
Simba walipata ushindi huo kwenye nusu fainali iliyochezewa uwanja wa Afraha, Nakuru.Walifika nusu fainali baada ya kuwaondoa Kariobangi Sharks wa Kenya.
Klabu hiyo sasa itamsubiri mshindi wa nusu fainali kati ya mabingwa wa ligi Kenya Gor Mahia na Singida FC ya Tanzania kufahamu nani atakuwa mpinzani wao fainali.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)