Pages

JAMII ISHIRIKISHWE MABADILIKO TABIA NCHI KUWA NA KILIMO CHENYE TIJA

 Mshehereshaji wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi, Mtafiti mshiriki wa ESRF, Abdallah Henku akitoa utambulisho wa wanenaji wa mdahalo huo uliofanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa ESRF.
 Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Meneja ushirikiano, uragibishi wa sera kutoka taasisi ya Food, Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network (FANRPAN) Bw. Lufingo Mwamakamba akizungumzia malengo ya warsha wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha Kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Muwasilishaji mada kutoka Taasisi ya CARE International nchini Malawi, Vitumbo Chinoko akiwasilisha mada kuhusu matumizi ya teknolojia katika kusaidia kuhifadhi mazingira wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha Kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Idara ya Menejimenti ya Mazingira Wizara ya Kilimo Bi. Shakwaanande Natai akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa sera ya kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha Kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa nchi kwenye mikutano ya mabadiliko ya tabia nchi kutoka ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Richard Muyungi akizungumzia vionjo vinavyotarajiwa kufanywa kuhusu uhifadhi wa mazingira na kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha Kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Muwasilishaji mada kutoka Taasisi ya CARE International nchini Malawi, Vitumbo Chinoko (wa pili kushoto) akifafanua kanuni za kufauta katika kuhifadhi mazingira na kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi wakati wa mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Idara ya Tafiti zilizoanishwa ESRF, Bi. Vivian Kazi (kulia), Mkurugenzi wa Sera, Mawasiliano na Uragibishi FANRPAN, Francis Hale (wa tatu kulia), Meneja ushirikiano, uragibishi wa sera kutoka taasisi ya Food, Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network (FANRPAN) Bw. Lufingo Mwamakamba (wan ne kulia) pamoja na Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango (kushoto) akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida.
Mkurugenzi wa Sera, Mawasiliano na Uragibishi FANRPAN, Francis Hale akifafanua jambo wakati majadiliano kwenye mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mshiriki akichangia mada wakati wa mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki kwenye mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Sera, Mawasiliano na Uragibishi FANRPAN, Francis Hale (katikati) akibadilishana mawazo na Muwasilishaji mada kutoka Taasisi ya CARE International nchini Malawi, Vitumbo Chinoko (kushoto) wakati wakielekea kwenye eneo la kupiga picha ya pamoja kwenye mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida.
 Picha ya pamoja ya washiriki wa mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
JAMII inayojitambua ndiyo inayoweza kutumika katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha  kushindikana kwa mipango mingi ya udhibiti wa uharibifu wa mazingira kunatokana na uelewa duni na mipangilio isiyozingatia mahitaji halisi ya wananchi wa maeneo husika.
Kauli hiyo imo katika Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ofisi za ESRF.
Katika mdahalo huo uliowezeshwa na Shirika la Kimataifa la Care kwa kushirikiana na taasisi ya FANRPAN na ESRF imeelezwa kuwa kuna changamoto kubwa kwa maendeleo ya kilimo na ukuaji wake kutokana na n chi nyingi Kusini mwa Afrika kutegemea mvua.
Aidha ilielezwa kuwa changamoto nyingine ni umaskini uliokithiri, upungufu nmkubwa wa raslimali watu, maandalizi hafifu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na miundombinu dhaifu.
Mmoja wa watoa mada kutoka Taasisi ya CARE International nchini Malawi, Vitumbo Chinoko alisema kwamba kumekuwa na kulegalega kwa matumizi ya teknolojia katika kusaidia kuhifadhi mazingira miongoni mwa wananchi na uwezeshaji kwa watendaji kiasi cha kuharibu muitikio unaonekana wakati wa mafunzo.
Chinoko alisema kwamba kutokana na hali hiyo walibuni kanuni ambazo wao wanaziita SUPER kanuni ambazo zikifuatwa vyema zinajibu matatizo yaliyopo sasa.
Alisema kwamba Super ni mfumo wa uchakataji wa taarifa na utekelezaji wake unaolenga kuwafikia wananchi wa pembezoni ambao ndio washiriki wakubwa wa utunzaji wa mazingira na uzalishaji wa chakula.
Alisema kwa kutumia kanuni hizo wananchi wanaweza kutambua mwendelezo wa rasilimali ardhi na misitu waliyonayo, wakawezesha kuitumia kwa faida kutokana na uadimu wake.
Aidha kanuni hizo zinahitaji mipango kuzingatia usawa wa kijinsia  ili kuteketeleza sera katika uchumi.
Alisema mfumo wa masoko unazungumzwa ikiwa ni pamoja na ushiriki wa sekta binafsi katika kilimo ili kuipaisha na kuifanya kuwa na tija zaidi.
Alisema kwa sasa kuna tatizo kubwa sana la kuwasilisha taarifa huku watengeneza sera wakiwa pekee yao bila kushirikisha wananchi ambao ndio watendaji wenyewe.
Katika mdahalo huo mada zingine ziliwasilishwa na Bi. Shakwaanande Natai, Mkuu wa Idara ya Menejimenti ya Mazingira Wizara ya Kilimo akishughulikia sera katika kilimo cha kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa nchini Tanzania.
Pia kulikuwa na mada iliyowasilishwa na Bw. Richard Muyungi kutoka ofisi ya Makamu wa Rais ambaye alizungumzia vionjo vilivyokusudiwa katika kuhakikisha wanazungumza kilimo kinachozingatia mabadiliko hali ya tabia nchi (INDCs) Tanzania.
Meneja ushirikiano, uragibishi wa sera kutoka taasisi ya Food, Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network( FANRPAN) Bw. Lufingo Mwamakamba alisema kwamba matokeo ya ushauri  katika mdahalo huo utafikishwa katika kanda na baadae dunia kwa kuwa utekelezaji wa mashauri hayo ni wa lazima kuzingatia mahitaji ya ulinzi wa mazingira kwa kuzingatia kilimo kinachoangalia mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema kwamba watatumia maazimio na ushauri kutoka katika mdahalo huo katika majukwaa mengine muhimu duniani ambayo yanazungumzia makubaliano ya COP 19 na maazimio ya Lome.
Alisema mdahalo huo ni muhimu katika kubaini utayari wa Tanzania na changamoto zake katika kuendesha kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi na kuhakikisha usalama wa chakula na lishe.
Alisema pamoja na kuwepo kwa sera nzuri za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kumekuwepo na hasara kubwa katika kilimo kinachofikia dola za Marekani milioni 200 duniani.
Alisema hasara hiyo ni tishio kwa maisha na kusema kwamba ni vyema wataalamu  naa wananchi wakazungumzia changamoto zilizopo kwa bara la Afrika ambalo linaweza kulisha dunia nzima kama mipango itachambuliwa ipasavyo kwa kushirikisha wananchi na wagani.
Alisema kilimo lazima kifanywe kwa kuzingatia mabadiliko ya hali ya tabia nchi ili kiwe na tija na kukabiliana na mafuriko, ukame, wadudu na magonjwa yanayotokana na mabadiliko hayo.
Bi. Shakwaanande Natai alisema kwamba Tanzania ipo tayari kufanya  kilimo cha kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa kutokana na kuwapo kwa sera na sheria zinazohimiza kilimo chenye tija.
Alisema mipango ya kilimo ya sasa inazingatia mabadiliko hayo pamoja na kutengeneza mfumo wa masoko ili kusaidia watu maskini kabisa wakulima kuwa na uwezo unaotakiwa katika kujisaidia kiuchumi.
Bw. Danford Sango akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida alisema kwamba mdahalo huo ni muhimu kutokana na mabadiliko ya tabia nchi kuwa tishio kwa ustawi wa wanadamu.
Aidha aliwakaribisha wataalamu kutoka nchi za Kusini mwa Afrika kushiriki katika mdahalo huo wenye tija kwa mataifa ya Kusini mwa Afrika.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)