Pages

Benki ya UBA Tanzania yaahidi neema katika Uchumi wa Tanzania

Dar Es Salaam, Tanzania. 1 June 2018. Benki ya UBA Tanzania imewatambulisha watendaji wake wakuu nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya Kubadilisha uongozi na kuleta Hamasa na mabadiliko katika Utendaji wake. Katika Kikao na waandishi wa habari kilichofanyika mapema Jumanne tarehe 29 May 2018 katika Ukumbi wa Lake Tanganyika uliopo katika Hoteli ya Hyatt Regency Watendaji hao wakuu akiwemo Mkurugenzi mkuu wa benki hio hapa Tanzania Bw Usman Isiaka na Mkurugenzi Mtendaji wa UBA Afrika Mashariki na Kusini Mwa Afrika Bw Emeke Iweriebor walipata nafasi ya Kujitambulisha.

Uteuzi wa watendaji hawa wa UBA ni moja ya mikakati yao kujiimarisha zaidi na kuchangia maendeleo ya uchumi wa Nchi . Usman amesema wana uzoefu mkubwa katika sekta  za kibenki wakiwa na zaidi ya miongo miwili na wanatarajia kutoa matokeo chanya katika uendeshaji wa benki Tanzania.Usman alikuwa kaimu mtendaji mkuu wa UBA Ghana kati ya mwaka 2014 hadi 2016.

Emeke Iweriebor ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa UBA Afrika mashariki na Kusini mwa Afrika ameeleza kwamba UBA GROUP imefanya maamuzi ya kuweka mikakati madhubuti ya kuongeza watendaji kwa ajili ya Afrika Mashariki na kusini mwa Afrika ili kuweza kuongeza ufanisi zaidi wa shughuli za kibenki katika kukuza uchumi wa Afrika kwa ujumla.

UBA Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika inajumuisha nchi za Tanzania ,Kenya,Uganda ,Congo DR, Mozambique na Zambia huku makao yake makuu yakiwa Jijini Nairobi.

Uwepo wa makao makuu Jijini Nairobi itasababisha kuwa karibu na wateja na kuweza kutoa huduma kwa ukaribu zaidi na kwa wakati pia kuwezesha mchango wao katika miundombinu ya maendeleo kama kilimo,umeme,barabara na,ujenzi.

Pia UBA inazidi kujiimarisha zaidi katika huduma za kimtandao za kibenki kwa wateja wake.UBA kwa sasa inafanya kazi katika nchi 20ikiwa pia na vituo vitatu vya kifedha kimataifa  vilivyopo London,Paris na New York.UBA imekuwepo Tanzania tangu mwaka 2009.
Kutoka kushoto ni Brendansia Kileo Mkuu wa Masoko na Mawasiliano,
Emeke Iweriebor  Mkurugenzi Mtendaji wa UBA Afrika Mashariki na Kusini 
mwa Afrika,Usman Isiaka Mtendaji mkuu wa UBA Tanzania,
Bwana Mathias Afisa Rasilimali watu Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Banki ya UBA imetambulisha watendaji wake wapya na kuelezea mipango yao katika kuchangia uchumi unaoendelea kukua nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)