Pages

WANAUZALENDO KWANZA KUSHIRIKI UZINDUZI WA KOMBE LA AWESO - PANGANI, TANGA

Wasanii wa Bongo Movie wanaunda kundi la Wanauzalendo Kwanza wakiongozwa na Mwenyekiti Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ (pichani) wanatarajiwa kwenda wilayani Pangani mkoani Tanga kuhudhuria uzinduzi wa Kombe la Aweso ikiwa ni pamoja na elimu na fursa mbalimbali za kuibua vipaji vya wasanii.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Steve amesema Jumamosi May 5, 2018 tutakuwa kwenye uzinduzi wa Kombe la Aweso lililoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Mhe. Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Mkuu wa Wilaya Ya Pangani Mhe. Zainab Abdallah leo lake ikiwa ni kuwaamsha vijana wajitokeze kupata elimu mbali mbali itakayokuwa ikitolewa.

"Tutakuwa wilayani humo wakiwaelimisha vijana juu ya kujitambua, kutumia fursa walizonazo kama kutumia vipaji walivyonavyo ili kufanikisha malengo yao ya kimaisha," amesema.

Ameongeza kuwa vijana wengi huvunjika moyo kutokana na changamoto wanazozipitia bila ya kujua watazitatua vipi, hivyo kupitia kampeni yao ya Amka Kijana wataweza kuwapa elimu.

Mbali na elimu hiyo pia amesema siku hiyo kutakuwa na mtanange wa soka baina ya mashabiki wa timu ya Simba na Yanga na baadaye watatembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vilivyomo wilayani humo.

Amesema wasanii mbalimbali kama, Aunt Ezekiel, Flora Mvungi, Jaqueline Wolper, Duma, Johari, JB na wengine wengi. Tamasha hilo litakuwa la wazi na halitakuwa na kiingilio.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)