Pages

RC DKT. KEBWE AAGIZA WAHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI GAIRO WAKAMATWE

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akipokea maelezo ya wizi wa pampu ya maji kutoka kwa mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe katika Kijiji cha Italagwe Kata ya Italagwe ili kuweza kuwalejeshea wanachi maji. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-GAIRO.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe  amesema nashangaa kuona pamoja na changamoto mliyonayo ya maji ila kuna watu bado wanahujumu miundo mbinu yenu jambo linakosesha majibu sahihi, walioiba Pampu hiyo ya maji hawajatoka nje ya kijiji cha Italagwe... naomba OCD ufanye msako wa nyumba kwa nyumba ili kubaini mwizi na pampu ipatikane mara moja.
Kisima kilichoibiwa pampu.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe wakielekea kukagua mradi wa maji uliokuwa unasumbua.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe wakitoa pole kwa wafiwa wilayani katika kijiji cha Tabuhoteli -Gairo wakati wa ziara yake ya siku tatu anayoifanya ili kuchochea maendeleo shughuli za maendeleo wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Tabuhoteli katika kata ya Chigela - Gairo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akitoa salamu zake kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Rachel Nyangasi akiwasalimia wananchi wa kata yake.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe wakiongoza wananchi kuelekea katika mradi wa maji wa Ihenje.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe wakipokelewa kwa ngoma.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe wakimsikiliza Mhandisi wa wilaya ya Gairo, Heke Bulugu wakati akitoa maelezo ya 
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe akitoa neno la shukrani.

Wananchi waliohudhuria.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Rachel Nyangasi akiwasalimia wananchi wa kata yake.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akizungumza na wananchi.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-GAIRO.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ameliagiza jeshi la Polisi Wilaya ya Gairo kuwatafuta na kuwakamata watu walioharibu miundo mbinu ya maji ikiwemo kuiba pampu ya maji ya Kijiji cha Italagwe katika Wilaya ya Gairo na kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria.

Dkt. Kebwe ametoa agizo mapema leo Mei 24 mwaka huu akiwa katika Kijiji cha Italagwe Kata ya Italagwe, wilayani humo wakati wa ziara yake ya siku tatu ya kutembelea na kuhimiza miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro.

Amesema kuwa changamoto kubwa inayowakumba wananchi wa Wilaya ya Gairo ni pamoja na tatizo la maji, hapati majibu sahihi kuona pamoja na changamoto hiyo bado kuna watu wanaodiliki kufanya hujuma ya kuiba miundo mbinu ya maji na kuwasababishia wengine kukosa maji.

"Nashangaa sana kuona pamoja na changamoto mliyonayo ya maji ila kuna watu bado wanahujumu miundo mbinu yenu jambo linakosesha majibu sahihi, walioiba Pampu hiyo ya maji hawajatoka nje ya kijiji cha Italagwe... naomba OCD ufanye msako wa nyumba kwa nyumba ili kubaini mwizi na pampu ipatikane mara moja," amesema.

“OCD Mkong’oto utembee kwenye kijiji hiki. Mkong’oto utembee pampu ipatikane. Kuna wengine watachukulia kisiasa siasa suala hili, hiyo ndiyo kazi ya Mbunge kuangalia kwamba tunachangamoto gani asaidiane na wananchi” alisema Dkt. Kebwe “wezi wapo hapa hapa kijijini. DC banana na Afisa Tarafa, Mtendaji wa Kata, Mtendaji wa Kijiji, fanyeni Mkutano wa hadhara pampu ipatikane” alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, mradi huo wa maji ulianza mwaka 2014 hadi 2015 ambapo uligharimiwa na Mbunge wa Jimbo la Gairo Mhe. Ahmed Shabiby na ulihudumia vitongoji viwili vya Dukani na Chang’ombe vyenye watu wasiopungua 2,500 na Oktoba mwaka 2017 mradi uposimama kutoa huduma kwa sababu ya pampu hiyo kuibiwa.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchemba amewahakikishia wananchi wa Gairo kuwa changamoto ya Maji wilayani humo inakaribia kuisha kwa kuwa takwimu pamoja na utekelezaji unaonesha upatikanaji wa maji unaongezeka. Upatikanaji wa maji mjini umeongezeka kutoka asilimia 35 hadi asilimia 40.7 na vijijini umefikia asilimia 51.4 kati ya asilimia 85 zinazohitajika hivyo mradi wa maji wa MORUWASA utakapokamilika changamoto ya maji Gairo itakuwa ni ndoto.

"Nawaomba wananchi wangu wa Gairo waendelee kuwa wapole maana kila kukicha tunajaribu kutatua changamoto zinazotukuta likiwemo hili la maji ambalo halitachukua muda mrefu tutakuwa tumelimaliza kabisa," amesema.

Mhe. Mchembe ameongeza kuwa wanawake wanaweza hivyo waendeee kuwaamini hawatawaangusha wananchi, "Wilaya yetu inaongozwa asilimia 70 inaongozwa na akinamama hivyo tunajua changamoto zinazokuba ikiwemo zile za majumbani... vumilieni yatakwisha'.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe bado anaendelea na ziara yake Wilayani Gairo kwa lengo la kutembelea na kuhimiza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kupokea kero za wananchi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)