Pages

Futari ya NMB kwa wadau na wateja Dar

Mkurugenzi wa NMB Bank ? Ineke Bussemaker akiongea katika futari iliyofanyika juzi jijini Dar es Salaam na kuhudhuria na wadau na Wateja wa NMB zaidi ya 200. NMB imekuwa na kawaida ya kufuturisha waumini wa Kiislam katika mwezi mtukufu wa Ramadan kwa kutambua umuhimu wa waislam kama sehemu ya Wateja wa benki hiyo. NMB Imepanga kutoa futari katika mikoa 8 ya Tanzania bara na mikoa miwili ya Zanzibar. 
Mkurugenzi wa NMB Bank ? Ineke Bussemaker akifuatilia hotuba kutoka kwa sheikh Mkuu wa Dar es salaam ? Alhad Mussa Salum wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na NMB Bank juzi jijini Dar es Salaam na kuhudhuria na wadau na Wateja wa NMB zaidi ya 200. NMB imekuwa na kawaida ya kufuturisha waumini wa Kiislam katika mwezi mtukufu wa Ramadan kwa kutambua umuhimu wa waislam kama sehemu ya Wateja wa benki hiyo.

BENKI ya NMB jana iliwafuturisha baadhi ya wadau na wateja wa NMB zaidi ya 200 Waislamu wakazi wa jiji la Dar es Salaam ikiwa ni utaratibu wake kuungana na wateja wake walioko katika mfungo mtukufu wa Ramadhan.

Akizungumza katika tukio hilo, Mkurugenzi wa Benki ya NMB ? Ineke Bussemaker alisema huo ni utaratibu wa kawaida kwa benki yake kufuturisha waumini wa Kiislam katika mwezi mtukufu wa Ramadan kwa kutambua umuhimu wa waislam kama sehemu ya Wateja wa benki hiyo.

Aidha aliongeza kuwa NMB imepanga kutoa futari kama hiyo katika mikoa 8 ya Tanzania Bara na mikoa miwili ya Zanzibar ikiwa ni kuungana na wateja wake waliopo katika mfungo mtukufu wa Ramadhan. Sehemu ya wateja wa NMB waliojitokeza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na NMB Bank juzi jijini Dar es Salaam na kuhudhuria na wadau na Wateja wa NMB zaidi ya 200. NMB imekuwa na kawaida ya kufuturisha waumini wa Kiislam katika mwezi mtukufu wa Ramadan kwa kutambua umuhimu wa waislam kama sehemu ya Wateja wa benki hiyo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)