Pages

AIRTEL NA VETA WASHIRIKIANA KUANDAA KONGAMANO LA ELIMU KUPITIA MTANDAO

Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano akitoa mada wakati kongamano la elimu kupitia mtandao yenye lengo la kuhamasisha kusoma kwa kujitengemea kwa miongoni mwa vijana hapa nchini kupitia teknologia ya VSOMO. Kongamano hilo liliandaliwa na Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Tanzania VETA na DTBi.
Godfrey Magila kutoka taasisi ya DTBi akitoa mada wakati kongamano la elimu kupitia mtandao yenye lengo la kuhamasisha kusoma kwa kujitengemea kwa miongoni mwa vijana hapa nchini kupitia teknologia ya VSOMO. Kongamano hilo liliandaliwa na Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Tanzania VETA na DTBi.
Mratibu wa VSOMO kutoka Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Tanzania VETA Charles Mapuli akitoa mada wakati kongamano la elimu kupitia mtandao yenye lengo la kuhamasisha kusoma kwa kujitengemea kwa miongoni mwa vijana hapa nchini kupitia teknologia ya VSOMO. Kongamano hilo liliandaliwa na Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Tanzania VETA na DTBi.
---
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Tanzania VETA wameshiriki kongamano la elimu kupitia mtandao yenye lengo la kuhamasisha ubunifu kwa vijana na kuonesha jinsi kijana anavyoweza kusoma kwa kujitengemea kwa kutumia ubunifu wa aplikesheni ya VSOMO inayotoa elimu kwa mtandao.

Kwa miaka miwili sasa, VETA kupitia applikesheni ya VSOMO imekuwa ikitoa elimu kupitia mtandao kwa wanafunzi ambao wanataka kupata elimu ya ufundi stadi kwa udhamini wa Airtel Tanzania.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kongamani hilo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema kampuni ya Airtel iliamua kuwa mmoja wa wadau wa teknolojia hii ya kutoa elimu ya VSOMO ikiwa ni moja wa mkakati wake wa kurudisha sehemu ya faida yake katika kusaidia Jamii. Kwa kuweza kutambua umuhimu wa Jamii inayotuzunguka, tuna miradi ya kusaidia vijana kujikwamua yenye lengo ya kuwapa vijana ujuzi ili wajiajiri au wapate ajira kwenye sekta mbali mbali ili kuunga mkono juhudi za serikali za kujenga uchumi wa viwanda.

Airtel Tanzania inayo furaha kuona kuwa matumizi ya smartphone yakiwa ni darasa au ikiwa ni moja ya njia ya kutumika kupata elimu ya ufundi. Hii haiukuwa rahisi kufanya peke yetu ndio sababu tuliamua kushirikiana na VETA kama taasisi ya serikali yenye mamlaka ya kutumia elimu ya ufundi hapa nchini huku DTBi wakiwa ndio waliombuni applikesheni ya VSOMO, alisema Singano.

Airtel na washirika wake VETA na DTBi kwa sasa wana utaratibu mpya wa malipo kwa awamu ili kuwezesha wanafunzi wanaotaka kupata elimu ya ufundi stadi kufanya bila kupata changamoto za kulipa karo, aliongeza Singano.

Mkuu wa chuo cha VETA Kipawa Injinia Sospeter Dickson Mkasanga alisema kuwa teknolojia imekuwa sana katika dunia ya leo na Tanzania kama nchi pia imefaidika sana. Kwa kutumia teknolojia, kila kitu sasa kinawezekana. Ni kwa kutumia teknolojia tumeweza kutoa elimu ya ufundi stadi kwa zaidi ya vijana 100 wakiwa hawapo darasani. Hii ni kitu ya kujivunia kwa sababu vijana hao wameweza kujiajiri na wengine wameajiri kwenye sekta mbali mbali kwa tunawakabidhi vyeti baada ya kumaliza elimu yao, alisema Mkasanga.

VSOMO imeweza kuwa mkombozi wa elimu ya ufundi stadi kwa kutumia teknolojia. Kwa kutumia simu za smartphone, wanafunzi wanapata ufundi stadi wa kozi yeyote wayohitaji. Naomba nitoe wito kwa vijana wote nchini ambao wangependa kupata elimu ya ufundi stadi wajiunge na wapakue applikesheni ya VSOMO kwani ni rahisi na pia malipo ya kozi ni nafuu, aliongeza Mkasanga.

Kwa upande wake, Godfrey Magila kutoka DTBi alisema kuwa ili kufanya teknolojia iwe na tija kwa Jamii, ni muhimu kwa Jamii kupata elimu ya umuhimu na matumizi ya teknolojia ili kufaidika nayo na pia kufanya baadhi ya mambo yawe rahisi katika maisha yao.

Jamii zetu zinapata changamoto kufikia malengo yao. Kwa sasa, teknolojia imekuwa kwenye vidole vyetu na ndio sababu watu wengi wanatumia smartphone ambazo zina uwezo wa kuweka memori kubwa. Kama Jamii yetu ingeweza kutambua na kuelewa elimu iliyopo kwenye smartphone hizo ingekuwa ni jambo la maana, alisema Magila.

Tangu kuzinduliwa kwa VSOMO Juni 2016, inaonyesha kuwa zaidi ya vijana 30,000 washapakua applikesheni ya VSOMO huku zaidi ya 10,000 wakijisajili na zaidi ya 100 wakiwa tayari washamaliza kusoma kupitia applikesheni hiyo na kukabidhiwa vyeti vyao.

Kozi ambazo ulitolewa ni Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo ya kompyuta, umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani , Umeme wa magari, Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi wa simu za mkononi, Ufundi Alluminium, Utaalamu wa maswala ya urembo pamoja ma Ufundi wa kuchomea vyuma.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)