Pages

OBC yatoa magari 15 kwa wizara ya maliasili

 Magari 15 yaliyokabidhiwa na Kampuni ya OBC ya Loliondo.

Mkurugenzi idara ya
wanyamapori, Nebbo Mwina akikata utepe kuashiria uzinduzi wa magari 15 aina ya
Toyota Land cruiser yenye thamani ya shilingi Billion 1.5 yaliyotolewa na
kampuni ya uwindaji ya OBC,ya Loliondo kwa ajili ya shughuli za kuzuia ujangili
na uhifadhi. Hafla hiyo ilifanyika jana jiji Dar es Salaam.



 Mkurugenzi idara ya
wanyamapori, Nebbo Mwina akijaribu kuendesha moja ya magari 15 aina ya Toyota
Land cruiser yenye thamani ya shilingi Billion 1.5 yaliyokabidhiwa  na
kampuni ya uwindaji  OBC,ya Loliondo kwa ajili ya shughuli za kuzuia
ujangili na uhifadhi. Hafla hiyo ilifanyika jana jiji Dar es Salaam
KAMPUNI ya uwindaji ya Otterlo Business Corporation Limited (OBC) imekabidhi magari 15 kwa wizara ya maliasili na Utalii kwa ajili ya kusaidia kulinda rasilimali ya wanyamapori nchini.

Magari hayo aina ya Toyota Landcruiser yalikabidhiwa jana kwa Mkurugenzi wa idara ya wanyamapori, Nebbo Mwina,katika ofisi za Wizara ya Maliasili, jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi magari hayo yenye thamani ya Zaidi ya sh. Bilioni 1.5, Mkurugenzi msaidizi wa OBC, Molloimet Yohana, alisema kuwa msaada huo ni mahususi kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye mapambano dhidi ya ujangili na ulinzi wa wanyamapori.

“Huu ni mwendelezo wa azma ya serikali ya UAE na OBC katika kuunga mkono mapambano hayo kwani tumekuwa tukifanya hivyo mara kwa mara,”alisema.

Alisema ushiriki wao katika uhifadhi wanyamapori utaendelea kwani ni mpango endelevu na kamwe hawatasita kusaidia pale itakapobidi.

Akipokea msaada huo, Mwina alisema serikali inatambua mchango mkubwa wa OBC ambao imekuwa ikitoa katika sekta hiyo,na kuwataka kuendeleza mahusiano na kutokatishwa tamaa na maneno yanayozungumzwa juu ya kampuni hiyo.

“Napenda kusema kwamba OBC tumekuwa na mahusiano na nyinyi ya muda mrefu tumepata misaada yenu kwa muda mrefu kwa hiyo mahusiano yenu na sisi ni ya muda mrefu na ni mazuri hivyo tunawaomba kwamba muendeze hayo mahusiano yenu msikate tamaa tunajua kuna maneno yanasemwahuku na kule yakijaribu kuwakatisha tamaa juhudi zenu naomba msikate tamaa kwa hayo maneno ambayo yanasemwa Chini chini “Alisema

Alisema ni vyema OBC ikawapuuza watu ambao wamekuwa wakisema kampuni hiyo hafanyi kazi yake inavyotakiwa lakini wao kama wizara tunatambua kwamba wamekuwa ni msaada msaada mkubwa kwa serikali na uhifadhi.

Akishukuru kwa msaada huo mkurugenzi wa mamlaka ya usimamizi wanyamapori nchini (TAWA )Dk. James Wakibara alishukuru OBC kwa msaada huo ambao alisema utarahisisha utendaji kazi wa mamlaka hiyo ambayo inakabiliwa na changamoto ya rasilimali fedha,watu na vifaa.

“Lazima tutoe shukrani zetu za dhati kwa uongozi wa OBC kwanza kwa kufikiria hili wazo lakini pia kwa kujitoa,nguvu waliyoifanya,jitihada walizozifanya,matumizi waliofanya hadi leo tunapata hivi vifaa ambavyo vitatusaidia mtufikishie salam zetu kwa mkurugenzi ambae hakuweza kufika lakini Mwambie tunashukuru na Tunaheshimu kwa msaada huu uliotolewa.”alisema

Amesema gari ni kitu mihimu sana katika shughuli ya uhifadhi kwa sababu inawezesha kufika mahali popote kwa kuwa ni vigumu sana kulinda mapori kwa kutembea kwa miguu.

“Ni vizuri kwamba mtu anapokusaidia lazima atakuwa amewaza hapa kuna tatizo kwa hiyo katika tatizo hili na mimi nisaidie,kwa hiyo ule moyo tu wa kusema kwamba niwasaidie wenzangu Ndio hazina kubwa kuliko hata kile kilichotolewa”,alisema Dk.Wakibara.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)