Pages

Mwalimu Rufiji ashinda pasaka mzuka jackpot ya milioni 260.


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akizungumza na wanahabari  mapema leo jijini Dar wakati wa kumtambulisha mshindi
Pasaka Mzuka Jackpot Edward Msenga (Kulia) na kumpongeza kwa ushindi mkubwa wa kujishindia kiasi cha Shiling Milion 260. Kushoto ni Mkaguzi kutoka michezo ya Bahati Nasibu  Bakari Maggid.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga  akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 260 kwa
mshindi wa Pasaka Mzuka Jackpot Edward Msenga .

Mshindi wa
Pasaka Mzuka Jackpot Edward Msengi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kutambulishwa na kushukuru kwa kupata fedha hizo na kuwataka watanzania waamini kuwa mchezo huo unatenda haki.



Tatu Mzuka, mchezo wa namba unaoongoza nchini leo umetangaza na kumtambulisha kwa wana habari mtanzania aliyebahatika kushinda milioni 260 kwenye Pasaka Mzuka Jackpot ambayo ilionyeshwa mubashara kupitia ITV, Clouds TV na TV 1 jumapili ya Pasaka.

Edward Msengi (56), ambaye anatokea Rufiji, Pwani ndiye aliyebahatika kuondoka na kitita cha shilingi milioni 260 ambayo ni jackpot kubwa kuwahi kutolewa kwa mshindi mmoja katika nchi hii.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Bwana Sebastian Maganga alimtambulisha mshindi na kumpongeza kwa ushindi huo mkubwa. “ Sisi Tatu Mzuka tunayo furaha kiasi kwamba tumeamua kumleta mshindi Dar es salaam ili kushiriki pamoja nanyi katika tukio hili kubwa” . Msengi ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Singida na baba wa watoto wanne alikuwepo kudhihirisha furaha yake na kuhadithia safari yake aliyopitia mpaka kushinda kitita kikubwa cha milioni 260.

“ Nimekuwa nikicheza Tatu Mzuka kwa muda sasa. Nina furaha kubwa sana. Sikuwahi hata kuota kama ningeweza kupata fursa kubwa kama hii. Ninategemea kujenga nyumba nzuri kwa ajili ya familia yangu na kuwekeza katika biashara pamoja na kuhakikisha kwamba watoto wangu wote wapo katika shule nzuri” alisema Bwana Msengi
 
Mbali ya tukio hilo adhim,Maganga aliufahamisha umma juu ya ujio wa  kampeni ya mwezi April ijulikanayo kama Mzuka FULL CHARGE.

“Maisha ni kusaidiana ndio maana unaposhinda Tatu Mzuka na kuwa ‘FULLCHARGE’; tunakupa fursa ya kumbusti mtu mwingine ambaye utamchagua. Shinda milioni 6 kila saa na upate nafasi ya kuingia kwenye jackpot ya milioni 10 kila siku na milioni 60 jumapili hii ili umbusti yoyote unayemtaka”

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)