Pages

MAHAKAMA YAINGIA MKATABA POSTA MLANGONI NA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe, akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba kati ya Posta na Mahakama ya Tanzania wa huduma ya Posta Mlangoni inayotolewa na shirika hilo. Hafla hiyo, imefanyika katika Ofisi za Mahakama ya Rufani, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga na kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa TPC, Zuhura Pinde. Waliosimama nyuma yao, ni baadhi ya Maofisa waandamizi wa Posta na Mahakama.
Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (kulia), akizungumza katika hafla hiyo,  jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe na katikati ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga. Wengine nyuma kutoka kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Fadya Zam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TPC, Elia Madulesi, Mtendaji wa Mahakama Kuu, Leonard Magacha, Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Solanus Nyimbi.
Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (kulia), akizungumza katika hafla hiyo,  jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe na katikati ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga. Wengine nyuma kutoka kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Fadya Zam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TPC, Elia Madulesi, Mtendaji wa Mahakama Kuu, Leonard Magacha, Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Solanus Nyimbi. 
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mwanasheria wa Mahakama ya Tanzania, Peace Mpango (kulia), akisaini mkataba huo, huku akiangaliwa kwa makini na Mwanasheria Mkuu wa TPC, Zuhura Pinde. 
Mwanasheria Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Zuhura Pinde, akisaini akisaini mkataba huo, huku akiangaliwa kwa makini na Mwanasheria wa Mahakama ya Tanzania, Peace Mpango.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga (kulia), wakibadilishana mkataba huo, mara baada ya kusainiwa katika hafla hiyo.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo, jijini leo.
Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika hafla hiyo.

CHINI NI TAARIFA YA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA ILIYOTOLEWA KWA VYOMBO VYA HABARI KATIKA HAFLA HIYO

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tunapenda kuwaarifu kuwa leo hii tarehe 5 April 2018 Shirika la Posta (TPC) litatiliana saini mkataba wa kutoa huduma za usafirishaji barua na nyaraka muhimu kati yake na Mahakama ya Tanzania .

Mkataba huo utashuhudiwa na kusainiwa na Postamasta Mkuu na mtendaji Mkuu wa Mahakama ambaye ameongozana na Maofisa Waandamizi. Katika Ofisi za Mahakama ya Rufani zilizoko Jijini Dar es salaam.

Mkataba huu chini ya huduma mpya ya Posta mlangoni(The post at your doorstep) iliyoanzishwa na Shirika la Posta hivi karibuni ,utalipa jukumu la kukusanya na kusafirisha barua zote na nyaraka mbalimbali za mahakama na kuzifikisha kwa wahusika kulingana na anwani zao na mahali walipo (Anwani za makazi).

Kusainiwa kwa mkataba huu kutawezesha kuongeza kasi ya barua za kawaida, ya Mahakama kuwafikia walengwa mapema zaidi kwani zitakuwa zinachukuliwa Mahakamani na maofisa wa Posta na kupelekwa moja kwa moja kwa wahusika/ muhusika.

Shirika la Posta litatumia uzoefu wake wa muda mrefu  kufanikisha jukumu hili, na hivyo kuzirahisishia mahakama zetu utendaji kwa kuwapunguzia mzigo wa ukusanyaji na usambazaji wa nyaraka zake hapa nchini.
Wito kwa Wananchi, tunawaomba watoe ushirikiano kwa maofisa wa Posta hususani kuandika anwani za makazi pamoja na postikodi.

Imetolewa na
Ofisi ya Uhusiano,Makao Makuu
Posta House, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)