Pages

CRDB Bank kupeleka wateja wake 24 kushuhudia fainali za kombe la Dunia, Urusi

Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa akionyesha vipeperushi vya kampeni mpya ya Benki hiyo kwa wateja wake, ijulikanayo kama #TwenzetuRussia, itakayowawezesha watumiajiwa kadi za malipo za TemboCard Visa za Benki hiyo kujishindia safari ya kwenda kuangalia mechi za michuano ya kombe la Dunia, zitakazofanyika nchini Urusi kuanzia mwezi Juni mwaka huu. 
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati akitangaza kampeni mpya ya Benki hiyo kwa wateja wake, ijulikanayo kama #TwenzetuRussia, itakayowawezesha watumiajiwa kadi za malipo za TemboCard Visa za Benki hiyo kujishindia safari ya kwenda kuangalia mechi za michuano ya kombe la Dunia, zitakazofanyika nchini Urusi kuanzia mwezi Juni mwaka huu. 

Benki ya CRDB leo imetangaza kuanza rasmi kwa kampeni ijulikanayo kama “Furahia kandanda murua nchini Urusi” #TwenzetuRussia, itakayowawezesha watumiaji wa kadi za malipo za TemboCard Visa za Benki hiyo kujishindia safari ya kwenda kuangalia mechi za michuano ya kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Urusi, kuanzia mwezi Juni mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki hiyo Bi. Tully Esther Mwambapa, alisema kuwa Benki ya CRDB imeanzisha kampeni kwa kushirikiana na kampuni ya Visa International ili kutoa fursa kwa wateja wake kwenda kushuhudia fainali hizo, ambazo huvutia hisia za watu wengi dunuani kote.

“Wateja wetu wenye TemboCardVisa, TemboCardVisa-Electron, TemboCard Visa-Gold, TemboCardVisa- Platinum na TemboCardVisa-Infinite, wakati wa kampeni hii watatakiwa kulipia bidhaa au huduma wanazonunua kwa kutumia TemboCardVisa zao kupitia mashine za malipo (POS) zilizopo sehemu mbalimbali kama kwenye migahawa, maduka, mahospitali, vituo vya mafuta na kwingineko, ili waweze kujishindia zawadi hii kubwa” alisema.

Bi.Mwambapa aliendelea kusema kuwa “iii mteja aweze kushinda, anatakiwa kufanya miamala mingi zaidi kila wiki na kadri mteja anavyolipia zaidi kwa kutumia TemboCardVisa yake, ndivyo anavyojiongezea nafasi kubwa zaidi ya kushinda.

Washindi wa wawili watakaokuwa wamefanya miamala mingi zaidi kila wiki watajishindia safari ya kwenda Urusi ambayo itagharamiwa kila kitu na Benki ya CRDB, ambapo jumla ya tiketi 24 zitatolewa” alisema Bi. Tully Mwambapa.

Bi.Mwambapa aliendelea kusema kuwa pamoja na washindi wawili wa kwanza kujishindia safari hiyo, Benki pia kila wiki itatangaza washindi wengine 10 kupitia vyombo mbalimbali vya habari ambao watajishindia zawadi kemkem ikiwemo luninga zitakazokuwa zimeunganishwa na kulipiwa kinga’muzi cha DSTV, jezi za timu za mataifa mbalimbali, mipira, kofia, fulana na na zawadi zingine nyingi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)