Pages

WANAWAKE MSD WATOA MSAADA HOSPITALI YA TEMEKE NA MAKAO YA WATOTO YATIMA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM

 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Amaani Malima akizungumza na Wanawake wa Bohari ya Dawa (MSD) waliofika Hospitalini hapo Dar es Salaam jana kwa ajili ya kutoa msaada wa vifaa vya kujifungulia na vitu vingine mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake MSD, Neema Mosha, Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Neema Mwela na Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Deodata Msoma.
 Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Neema Mwela, akimkabidhi Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Amaani Malima,  Mfuko wenye vifaa vya kujifungulia akina mama (Delivery Pack)
 Wanawake wa MSD wakiwa katika picha ya pamoja na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Amaani Malima baada ya kupokea msaada huo.
 Kutoka kushoto ni  Florence, Agatha na Naomi wakifurahia jambo wakati wakiwa nje ya wodi ya wazazi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke wakisubiri kutoa msaada huo.
 Wanawake wa MSD, wakiwa nje ya wodi ya wazazi wakisubiri kutoa msaada.
 Hapa wakiwa na Mifuko yenye vifaa vya kujifungulia akina mama (Delivery Pack) tayari kwa kwenda kukabidhi wodini.
 Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Deodata Msoma akiwaekeza jambo Wanawake wa MSD wakati akiwakaribisha wodini kwenda kutoa msaada huo.
 Wakina mama na baba wakiwa nje ya wodi ya wazazi na watoto wao katika hospitali hiyo.
 Vifaa vikiwa vimebebwa tayari kwa kutolewa kwa wajawazito.
 Maboksi yenye vifaa hivyo yakishushwa kwenye gari.
 Safari ya kwenda wodini kutoa msaada huo.
 Hapa wakiserebuka Makao ya Taifa ya Kurasini ya Kulelea Watoto Yatima na Wenye Shida.
 Wakijumuika na watoto wanaoishi kwenye makao hayo.
 Baadhi ya mifuko yenye chakula vilivyo tolewa.
 Kaimu Ofisa Mfawidhi wa Makao hayo, Happyness Nyange akizungumza na wanawake wa MSD.
  Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Neema Mwela, akimkabidhi msaada wa vyakula na vitu vingine Kaimu Ofisa Mfawidhi wa Makao hayo, Happyness Nyange. Kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa MSD, Neema Mosha.
 Msaada huo ukitolewa
Picha ya pamoja.

Na Dotto Mwaibale

WANAWAKE Wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD), katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani wametoa msaada wa vifaa vya kujifungulia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke pamoja na chakula kwa watoto wanaolelewa Makao ya Taifa Kurasini ya Watoto Yatima na Wenye Shida jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD,  Neema Mwela alisema kwao ni faraja kubwa kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani kwa kuwatembelea wanawake wenzao katika hospitali hiyo pamoja na watoto hao.

"Sisi wanawake wa MSD tuliona ni vizuri tukasherehekea siku yetu pamoja na wakina mama waliopo katika hospitali hii pamoja na watoto wanaolelewa katika makao ya taifa ya Kurasini kwa ajili kula nao chakula cha mchana pamoja na kuwapa msaada wa chakula na vitu mbalimbali" alisema Mwela.

Mwela alisema katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke waliweza kutoa Mfuko wenye vifaa vya kujifungulia akina mama (Delivery Pack) ambao umepunguzwa bei kutoka shilingi 40,000 mpaka shilinhi 21,000 na vifaa vingine vinavyohitajika kama sabuni na miswaki.

Akizungumzia watoto Yatima na wenye shida wanaolelewa katika makao ya Kurasini alisema ni jukumu la kila mmoja wetu kuwasaidia watoto hao badala ya kuiachia serikali pekee.

Alisema kazi ya malezi ya watoto hao ni kubwa mno hivyo kila mtu anapaswa kuwa na majukumu ya kuwalea kwani kumlea mtoto tangu akiwa mdogo hadi kufikia miaka 18 ni kazi kubwa.

Kaimu Ofisa Mfawidhi wa Makao hayo, Happyness Nyange alisema katika makao hayo kuna watoto wanaosoma shule mbalimbali za msingi, sekondari na shule za awali na kuwa kama kuna mtu anayehitaji kumchukua mtoto wa kwenda kuishi naye taratibu zote zinaanzia ofisi za ustawi wa jamii zilizopo kwenye manispaa husika.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa MSD, Neema Mosha alisema waliguswa sherehe za siku ya wanawake duniani mwaka huu kuwatembelea wanawake wenzao waliopo wodi ya wazazi kwa ajili ya kujifungua pamoja na kula chakula na watoto Yatima na wale wenye shida waliopo Kurasini na kuwapa msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali vya matumizi ya shule.

Alisema fedha za kununulia mahitaji hayo zilichangwa na wao pamoja na wafanyakazi wanaume wa MSD na kuwa thamani ya fedha kwa ajili ya kununulia vitu hivyo ilikuwa ni shilingi milioni 3.5 wakati vifaa vya hospitalini viligharimu shilingi milioni 7.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Amaani Malima alishukuru kwa msaada huo nakuleza kuwa changamoto kubwa walionayo ni majengo ya hospitali hiyo kuwa machache kutokana na ongezeko la wagonjwa na uboreshaji wa miundombinu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)