Pages

Waliomaliza Shule ya Msingi Bunge 1997 watoa msaada wa viti 20 kwa shule hiyo



Umoja wa Wanafunzi waliomaliza Shule ya Msingi Bunge mwaka 1997 iliyopo Ilala Jijini Dar es Salaam wametoa msaada wa viti 20 kwa shule hivyo ambayo vitatumiwa na walimu ambao wanafundisha katika shule hiyo.

Akizungumza kuhusu msaada huo, Mwenyekiti wa umoja huo, Bernard Chezue alisema msaada huo ni sehemu ya shukani yao kwa shule hiyo kwa kuwapatia eleimu ambayo imewasaidia kimaisha mpaka sasa wakiwa na mafanikio.

Alisema wamejipanga kuhakikisha wanaendelea kuisaidia shule hiyo ili iwe na mwonekano mzuri jambo ambalo litachochea wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa bidii.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi ambao walisoma Shule ya Msingi Bunge na kumaliza mwaka 1997, Bernard Chezue akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi viti 20 kwa uongozi wa shule ya Bunge.


"Tumekabidhi vitu hivi sabau tunaona tuna umuhimu wa kusaidia kwa sababu tumsoma hapa na sisi tumekuwa na mafanikio kwa kupitia shule hii, tumekuja kutoa shukrani kwa waliu wetu na shule kw ujumla,

"Huu ni mwanzo tu tutaumika nafasi yetu kutoa misaada zaidi na zaidi kwa namna Mungu anavyotujalia maana kuja kupata rangi, kubadilisha madarasa na hata baadae kuja kutoa zawadi kwa wanafunzi wanaofanya vizuri," alisema Chezue.

Pia Chezue aliwataka watu wengine ambao walisoma katika shule hiyo kuungana kwa pamoja na kusaidia mahitaji mbalimbali ambayo yanahitajika shuleni hapo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge, Radhia Mfalingundi akitoa neno la shukrani kwa Umoja wa Wanafunzi ambao walisoma Shule ya Msingi Bunge na kumaliza mwaka 1997 kwa kutoa msaada wa viti 20 kwa shule hiyo.
Nae Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge, Radhia Mfalingundi aliwashukuru wanafunzi hao kwa kutambua kuwa bila shule hiyo yanawezekana wasingekuwa na mafnikio hayo lakini pia kuwataka kuendelea kuwa na moyo huo wa kuisaidia kwa mahitaji mbalimbali.

"Nimefarijika sana na wanafunzi waliomaliza mwaka 1997 kutuletea msaada, kwamba wametambua mwalimu ni hazina na mafinikio waliyoyapata yametokana na mwalimu na wameona ni vyema wawasaidie wadogo zao ili na wao wafanikiwe kama wao walivyofanikiwa,

"Tunaamini watakuja tena kufanya vitu vikubwa sana sababu msingi waliopata katika maisha yao walipata katika Shule ya Msingi Bunge hivyo tunaamini wameamini mafanikio yao yametokana na shule hii," alisema Mfalingundi.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi ambao walisoma Shule ya Msingi Bunge na kumaliza mwaka 1997, Bernard Chezue akimkabidhi kiti Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge, Radhia Mfalingundi. Umoja huo umetoa msaada wa viti 20 katika shule hiyo.
Wanachama wa Umoja wa Wanafunzi ambao walisoma Shule ya Msingi Bunge na kumaliza mwaka 1997 wakiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule ya bunge.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)