Pages

TATU MZUKA YAKABIDHTI KALENDA 500 KWA JESHI LA POLISI,IGP SIRRO ATOA NENO

Kampuni ya Bahati Nasibu Tatu Mzuka imekabidhi kalenda 500 kwa Jeshi la Polisi  nchini,kama mwanzo wa uhusiano mwema utakaozaa matunda kati ya Tatu  Mzuka na Jeshi la Polisi. 

Akizungumza na waandishi habari wakati makabidhiano ya kalenda kwa Jeshi la Polisi  mapema jana , Msemaji wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga amesema wameamua  kutengeneza kalenda 500 za Jeshi la Polisi kama sehemu ya kujenga  uhusiano bora, lakini pia kuendeleza kauli mbiu ya Tatu Mzuka ya  ukishinda Tanzania inashinda pia. 

Maganga amesema wao ni raia wema wa Tanzania hivyo ni nafasi ya pekee kuwa  mbele kutokana na kazi ambayo inafanya jeshi la Polisi katika kulinda
watu na mali zao chini ya Mkuu wa Jeshi la Polisi(IGP), Simon Sirro,na
kwamba 
Kauli mbiu ya Tatu Mzuka “Ukishinda Tanzania inashinda”, 

“Mchezo wa bahati nasibu wameweza kushirikiana na Mkuu wa wilaya ya Temeke  katika kusaidia ujenzi wa kituo cha polisi kuwasaidia wananchi wa Mbande baada ya mapolisi kuuliwa kwa kutokuwa na kituo maeneo ya karibu. " Tumefanya kitu hiki kwa niaba ya washindi wa mchezo wetu wa bahati  nasibu,ambao mpaka sasa wamefikia idadi ya milioni 6 ambao wote
wamehakikishiwa usalama wao na jeshi la polisi.

Mkuu wa jeshi la Polisi ( IGP ) Simon Sirro ameeleza kuukubali mchezo wa kubahatisha nchini wa Tatu Mzuka unaoshika kasi kwa kubadilisha maisha ya Watanzania wengi. 

IGP Sirro amesema hayo wakati akipokea kalenda za jeshi hilo  zilizokabidhiwa na viongozi wa Tatu Mzuka kwenye makao makuu ya Jeshi la Polisi, Posta jijini Dar es Salaam juzi."Mmefanya jambo  jema lakini pia mmeonyesha mfano kwa wengine, binafsi nimeguswa na  mwamko wenu, hongereni sana na endeleeni kuchapa kazi," alisema IGP  Sirro. 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akikabidhiwa moja ya Kalenda kati ya 500 zilizotolewa na Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya Tatu Mzuka,kutoka kwa Mratibu wa Mawasiliano kampuni hiyo Sebastian Maganga (pichani kati).kulia ni Mmoja wa Wakilishi Simon Simalenga.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akikabidhiwa moja ya faluna ya Tatu Mzuka kutoka kwa  Mratibu wa Mawasiliano  Tatu Mzuka, Sebastian  Maganga (pichani kati).kulia ni Mmoja wa Wakilishi Simon Simalenga.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)