Pages

FAILUNA AIBEBA TANZANIA KILI MARATHON, ASHINDA MEDALI YA FEDHA

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. milioni 1, mshindi wa pili wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon Kilometa 21, Failuna Abdi, ambaye ni mtanzania pekee aliyeibuka mshindi kati ya Wakenya 9 katika mbio hizo zilizofanyika Moshi mkoani KilimanjaroNa Ripota wa Mafoto Blog, Moshi. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO
***************************************************
Nyota wa riadha, Failuna Abdi Matanga ameibeba Tanzania kwenye mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon zilizofanyika jana mjini Moshi na kuwakusanya mamia ya wapenda riadha katika moja ya matukio makubwa ya riadha nchini.
Failuna aliwaduwaza Wakenya kwenye mbio za Tigo nusu marathoni (kilomita21) alipomaliza wa pili akitumia saa 01:13:52 sekunde sita nyuma ya Mkenya, Grace Kimanzi aliyeibuka kinara akikimbia kwa saa 01:13:46 huku Pauline Rkahenya akimaliza wa tatu akikimbia kwa saa 01:13:54.
"Nilitarajia dhahabu, nilimuacha mpinzani wangu njiani, lakini alikuja kunipita mwishoni baada ya kuongeza mwendo.
" Nafarijika kuona nimeshinda medali ya pili, hii ni zawadi kwa Watanzania," alisrma Failuna muda mfupi baada ya kumaliza mbio kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika, Moshi.
Upande wa wanaume nafasi ya kwanza hadi ya 10 ilichukuliwa na Wakenya walioongozwa na Geofrey Torotich, Simon Muthoni alimaliza wa pili na Shedrack Korir alihitimisha tatu bora.
Kwenye mbio za Kilimanjaro  Premium Lager marathoni (kilomita 42) nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Cosmas Mutei, wa pili ni Elikana Yego na George Nyamure alimaliza wa tatu wakati kwa wanawake bingwa ni Flavious Teresa, Dorice Omary alimaliza wa pili na Sylivia Tenai wote kutoka Kenya alihitimisha tatu bora.
WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. milioni 4, mshindi wa kwanza wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon Kilometa 42, Cosmas Muteti, katika mbio hizo zilizofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro,leo.
*******************************************
Wadhamini wa mbio hizi ni Kilimanjaro Premium Lager-42km, Kampuni ya Simu ya Tigo-21km na Grand Mal5km,. Wengine ni First National Bank, Kilimanjaro Water, Diamond Motors Ltd, Kibo Palace, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, Simba Cement, KNAUF Gypsum na katika masuala AAR  ambao ni wabia ya matibabu na inaandaliwa na Wild Frontiers na DeepBlue Media na kuratibiwa na kampuni ya Executive Solutions.
Mapema jana Waziri Mwakyembe alikuwa miongoni mwa viongozi walioshiriki mbio za Grand malt kilomita 5 ambapo alizianzisha saa 01:30 Asubuhi na yeye akamaliza kukimbia saa 02:05 Asubuhi.
Mwakyembe ambaye aliongozana na Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) aliwapongeza waandaaji wa mbio hizo, sanjari na wadhamini wote walioshiriki kuzifanikisha huku akisisitiza kuwa kwa hamasa aliyoiona inatoa taswira nzuri ya Tanzania kwenye riadha.
"Sijui hata nisemeje, lakini waandaaji wa mbio hizi na wadhamini wake wanahitaji pongezi ya hali ya juu, sijawahi kuona mbio yenye mashabiki wengi namna hii, kwa hamasa hii naiona Tanzania katika ramani nyingine ya riadha kupitia Kili marathoni na miseme tu kwenye mbio za 2019 yatatokea mapinduzi makubwa, yasipotokea basi mimi nitatafuta kazi ya kufanya," alisema Waziri Mwakyembe.
Meneja Masoko, Udhamini, Habari na Promosheni wa TBL, George Kavishe, aliyemwakilisha Mkuugenzi wa Masoko, Thomas Kamphuis, alisema wao kama wadhamini wakuu kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager, wanafarajika kuwa sehemu ya mafanikio wa mbio hizi tangu kuanzishwa kwake na kuongeza kuwa wataendelea kutoa ushirikiano kama wadhamini wakuu kwa miaka 16 mfulululizo.
“Umati huu leo ni ishara tosha kuwa mashindano haya yamekuwa na sisi kama wadhamini tunafarajika kuendelea kushirikiana na Kilimanjaro Marathon,” alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema udhamini wao wa kilometa 21 umekuwa na manufaa makubwa kwani wameweza kujitangaza na kufanikiwa kuwa kampuni yenye mtandao wa 4G imara kabisa kuliko mitandao mingine.
Tigo pia ilitumia fursa hiyo kusitisha namba ya mwanariadha maarufu, Joram Mollel maarufu kama ‘Babu” 1040 kama heshima kwake na kusema namba hii haitatumika na mtu mwingine tena.
Mbio hizo zilishirikisha wanariadha zaidi ya 10,000 wakiwamo nyota wa zamani, Filbert Bayi, John Stephen Akhwari, Zacharia Barie, Juma Ikangaa na Gidamis Shahanga ambao walihusika kwenye masuala mbalimbali ya kiufundi.
Bingwa wa mwaka huu wa marathoni aliondoka na kitita cha Sh 4milioni kwa wanaume na wanawake wakati kwenye nusu marathoni bingwa aliondoka na Sh 2 Milioni.
 Mshindi wa pili wawa mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon Kilometa 21, Failuna Abdi, ambaye ni mtanzania pekee aliyeibuka mshindi kati ya Wakenya 9 katika mbio hizo zilizofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro leo, akiinua hundi yake ya Sh. milioni 1 baada ya kukabidhiwa.
 Mshindi wa kwanza wa mbio za Kilimeta 42, Cosmas Muteti, kutoka nchini Kenya akimaliza mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro 
 Mshindi wa kwanza wa mbio za Kilimeta 21, Geofry Torotich, kutoka nchini Kenya akimaliza mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro
 Baadhi ya washiriki wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon, kati ya washiriki wa mbio hizo 11, 0000 wakianza kutimua mbio kuanzia katika uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi, mkoani Kilimanjaro 
 Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, akizindua mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon Kilometa 21 zilizofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro 
 Kilometa 21 wakianza kutimua mbio
 Mshindi wa kwanza wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon Kilometa tano, Bazil Sule, kutoka Polisi Arusha akimaliza mbio hizo katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro,
Washiriki wa mbio za Kilimeta tano za Grand Mart Kilimanjaro Premium Lager Marathon, wakimalizia mbio hizo katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)