Pages

AIRTEL YAFUNGUA OFISI WILAYA YA GAIRO

HATIMAYE Kampuni ya Simu ya Airtel yawatendea haki wana Gairo.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Airtel.

Kwa kiasi kikubwa mtandao wa Airtel ndio mkombozi mkubwa wa wananchi wa Gairo hasa vijijini. Bado mawasiliano  ya simu ni changamoto kubwa sana Gairo.Mhe. Mchembe aliendelea kuwapongeza Airtel kwa ajira zaidi ya 400 nchini kupitia ofisi zinazozinduliwa sasa. Vijana wa Gairo pia ni wafaidika wa Ofisi hizo.

Kabla ya kufunguliwa ofisi hizo, wananchi walikuwa wanaenda Dodoma au Morogoro kwa huduma mbalimbali zinazohitaji kushughulikiwa na Airtel wenyewe.Mhe. Mchembe anayakaribisha mashirika mengine ya simu kufungua ofisi Gairo. Wilaya inakuwa kwa kasi kubwa na mzunguko wa pesa ni mkubwa na mawasiliano yanahitajika kwa kasi kubwa.
 Picha ya Pamoja mara baada ya kuzindua duka Wilayani Gairo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe(Kulia) akilishwa keki wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Airtel Wilayani Gairo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)