Pages

Watanzania watakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki Kili Marathon

Wadhamini wa Kilimanjaro Premium Lager Marathon wametoa wito kwa watanzania na washiriki wengine kuhakikisha wanajiandikisha mapema ili kushiriki katika mbio za mwaka huu ambazo zinatarajiwa kuwa kubwa zaidi na kuwavutia watu wengi zaidi ikilinganishwa na mwaka jana.
Rai hii inakuja takriban wiki mbili kabla kufanyikakwa mbio hizo maarufu ndani na nje ya nchi ambazo huwaleta pamoja zaidi ya washiriki 10,000 kutoka nchi zaidi ya 45 mjini Moshi ambapo mbhio hizi hufanyika.
Akizungumza jinini Dar es Salaam,Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli, ambaye bia yake ndio mdhamini mkuu, alisema tayari usajili umeshafunguliwa na kuwataka washiriki hususan wale wa mbio za kilometa 42 zinazodhaminiwa na bia hiyo, kujisajili kwa wingi ili Milioni 20 walizotenga za zawadi zibaki Tanzania.
“Bila shaka tunatarajia kuwa mbio za mwaka huu zitakuwa kubwa zaidi ndio maana tunasisitiza kuhusu usajili mapema ili kuepuka usumbufu dakika za mwisho,” alisema huku akiwapongeza waandaaji kwa maandalizi mazuri huku wakazi wa Dar es Salaam wakipewa nafasi ya kujisajilipia Februari 24 na 25 katika viwanja vya Mlimani City.
Alisema wao kama wadhamini wakuu pia watatoa milioni moja kwa mTanzania wa kwanza wa katika mbio za kilometa 42 na milioni moja pia kwa mwanamke. “Hii ni mojawapo ya njia za kuongeza hamasa katika mbio hizi ambazo miaka ya nyuma zimetawaliwa na Wakenya."
Meneja Masoko wa Grand Malt Warda Kimaro akizungumza kuhusu Kili Marathon.
Naye kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo alitoa wito kwa washiriki wote wa kilometa 21 kuanza maandalizimapema ikiwemokujisajili tayari kwa mbio hizo zitakazofanyika Moshi Machi 4 katika Cuo Kikuu cha UshirikaMoshi (MoCU).
“Mbio zetu za kilometa 21 zimekuwa maarufu zaidi na tunasisitiza kuhusu kujisajili mapema ili tuwe na washiriki wengi zaidi mwaka huu na kuendelea kutuunga mkono Tigo katika kufanyambioza kilometa 21 kuwa maarufu zaidi,” alisema na kuongeza kuwa wametenga milioni11 kwa ajili ya zawadi.
Meneja Masoko wa Grand Malt, Warda Kimaro ambaye kinywaji chake kinadhamini mbio za kilometa 5maarufu kama fun run, alisema mbiohizi zimekuwa maarufu sana kwani zinahusisha watu wa rika zote huku akiwataka wajisajili mapema kabla ya kufika Moshi ili waepuke usumbufu.
Wadhamini wengine katika mbio hizi ni First National Bank, Kilimanjaro Water, Diamond Motors Ltd, Kibo Palace, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, Simba Cement, KNAUF Gypsum na AAR as ambao ni wabia katika masuala ya tibabu.
Usajili Arusha utafanyika Februari 27 na 28 katika hoteli ya Kibo Palacekuanzia saa nane mchana hadi saa kumi na moja na Moshi ni Machi 1 kuanzia saa sita mchana hadi saa moja usiku, Machi 2 kuanzia saa nne asubuhi hadi saa moja jioni na Machi 3 kuanzia saa tatu hadi saa sita mchana.
Kilimanjaro Marathon, ambayo mwaka huu itafanyika Machi 4 katika viwanja vya MoCU, huandaliwa na Wild Frontiers na Deep Blue Media na kuratibiwa kitaifa na kampuni ya Executive Solutions.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)