Pages

Tatu Mzuka yazindua kampeni ya Valentine, ‘Ukishinda, Unayempenda naye Anashinda’

 Mkuu wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Sebastian Maganga,akizungumza mapema leo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu kampuni hiyo kuzindua kampeni  mpya ya Valentine  ‘Ukishinda, Unayempenda naye Anashinda’  , ambayo inaanza rasmi leo hadi februari 18,2018.Pichani kulia ni Msanii wa muziki wa kizazi kipya aitwae Nandy pamoja na Aslay (kushoto) ambao wamechaguliwa kuwa mabalozi wa kampeni hiyo
 Msanii mahiri wa Muziki wa Kizazi kipya Aslay akighani moja ya wimbo walioimba pamoja na msanii mwenzake aitwaye Nandy 'subah lakheri' kama sehemu ya kionjo kwa wanahabari walioshiriki mkutano huo mapema leo jijini Dar.
 Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye mkutano huo
 Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Aslay na Nandy kwa pamoja wakiimba wimbo wao wa 'subah lakheri'mbele ya wanahabari waliofika kwenye mkutano huo mapema leo jijini Dar
 Picha ya pamoja


• Zaidi ya milioni 300 kutolewa katika msimu huu wa Valentine

 Kampuni ya mchezo wa bahati nasibu, Tatu Mzuka, leo wamezindua kampeni mpya ya Valentine, ambayo inaanza rasmi leo hadi tarehe 18 ya mwezi wa pili.

Kampeni hiyo yenye kauli mbiu, ‘Ukishinda, Unayempenda Naye Anashinda’ imelenga kuhakiksha inashamirisha msimu wa Valentine kwa watanzania kupata fursa ya kujishindia mamilioni lakini pia wawapendao pia kupata fursa ya kushinda.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, bwana Sebastian Maganga, alisema Tatu Mzuka imekuwa na utaratibu wa kuwa na kampeni zinazoendana na misimu ya sherehe za kitanzania.

‘Kwa msimu huu wa Valentine peke yake, zaidi ya shilingi MILIONI 300 zitatolewa kwa washindi wetu watakaocheza kuanzia tarehe 1 hadi 18 ya mwezi huu’ alisema Maganga.

Kama sehemu ya kampeni hiyo pia, Maganga alisema pia KILA SIKU kwa siku 18 kiasi cha MILIONI 10 zitakuwa zinatolewa, ambapo MILIONI 5 itakuwa ya mshindi na MILIONI 5 itakuwa ya mtu ambaye mshindi atamchagua.

‘Lakini pia kubwa kuliko, ukicheza kuanzia leo hadi tarehe 18 utapata pia fursa ya bure kuingia kwenye Valentine SUPA MZUKA Jackpot, ambapo mamilioni yatatolewa kwa washindi, ambapo pia mamilioni ya ziada yatakwenda kwa wanaowapenda’ alisema Maganga.

Kwa upande mwingine, Maganga aliwatambulisha Aslay na Nandy kama mabalozi wa kampeni hii, ambao pia watakuwa na matamasha makubwa katika msimu huu wa Valentine ambayo yatafanyika katika mikoa ya Tanga, Arusha na Dar.

‘Tunaomba mashabiki wetu wacheze Tatu Mzuka katika kipindi hiki, kwani wakishinda pia watapata fursa ya kuhudhuria matamasha yetu pamoja na kukaa sehemu ya watu maalumu pia watapata fursa ya kupiga picha na sisi na mambo mengine kibao’ alisema Aslay.

Akizungumza katika uzinduzi huo, msanii Nandy alisema anaamini kila mtu ana mtu anayempenda na ndio maana amefurahia kampeni hii kwani inawakumbusha watannzia misingi yetu ya upendo.

Namna ya kucheza Tatu Mzuka kipindi hiki cha Valentine ni rahisi kwa kutuma shilingi 500 hadi 30,000 kwenda namba ya kampuni 555111, na kumbukumbu namba ni namba zako tatu za bahati zikufuatiwa na neno PENDA, na hiyo itakupa fursa za kushinda kila saa, kila siku na pia kuingia kwenye SUPA MZUKA JACKPOT pamoja na kupata fursa ya kuhudhuria matamasha ya Nandy na Aslay.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)