Pages

SERIKALI NA SHIRIKA LA THAMINI UHAI WAZINDUA KAMPENI YA MATUMIZI BORA YA HUDUMA ZA UZAZI NA WATOTO , KIGOMA

Mkuu wa mkoa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga (katikati mwenye kotI jeusi) na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la thamini Uhai Dk.Nguke Mwakatundu (wa pili kulia) wakikata utepe kuashiriki uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo,wengine ni wadau wa afya mkoani Kigoma.
Mkuu wa mkoa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Thamini Uhai, Dk.Nguke Mwakatundu (katikati ) akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Baadhi ya wadau wa afya mkoani Kigoma wakati wa uzinduzi huo
---
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Shirika la Thamini Uhai imezindua kampeni ya “Mjamzito na Mtoto Salama ni Wajibu Wetu” kupitia radio na uhamasihaji jamii kwa lengo la kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto mchanga mkoani Kigoma.

Kampeni hii ina lengo la kuhamasisha akina mama kwenda kujifungua katika vituo vya afya,kupanga na kujiandaa kujifungua, na kuweza kutambua dalili hatarishi kipindi cha ujauzito na kuweza kutafuta huduma ya haraka wakati dalili hatarishi zinapojitokeza.

Kampeni pia inakuza mpango shirkishi wa uzazi katika vituo vya afya kadhaa vilivyochaguliwa Kigoma. Mpango huu utahimiza akina mama kuja na msindikizaji wa kike atakayemsaidia mama mjamzito kipindi anapokuwa chumba cha kuzalia.

Vikwazo vingi vya afya, na vingi vinavyohatarisha afya ya mama na mtoto huweza kutokea kipindi cha awali. Hivyo basi kujifungua katika vituo vya huduma za afya ni njia salama ya kulinda afya ya mama na mtoto. Na hii sio kwa akina mama wenye ujauzito hatarishi pekee lakini pia kwa akina mama wajawazito wote kwa sababu matatizo yasiyotarajiwa yanaweza kutokea hatua yoyote wakati wa mchakato wa kujifungua.

Kwa mujibu wa utafiti wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuhusu Idadi ya Watu na Afya,Tanzania asilimia 47 tu ya wanawake mkoani Kigoma hujifungua katika kituo cha huduma za afya.

Thamini Uhai ni shirika lisilo la kiserikali nchini Tanzania ambalo linasaidia juhudi za kitaifa kupunguza vifo vya uzazi nchini Tanzania tangu mwaka 2008.Inafanya kazi na serikali ya Tanzania na Thamini Uhai ni shirika lisilo la kiserikali nchini Tanzania ambalo linasaidia juhudi za kitaifa kupunguza vifo vya uzazi nchini Tanzania tangu mwaka 2008. Inafanya kazi na serikali ya Tanzania na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali

Thamini Uhai hujenga uwezo wa kutoa huduma ubora, salama na upatikanaji wa huduma mtambuka ya dharura ya uzazi (EmonC), katika vituo vya serikali,i kwa sasa inasaidia vituo vya afya 50 katika mkoa wa Kigoma.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mheshimiwa Brigadier Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga,alisema kwamba kampeni hii inaendana moja kwa moja na mpango wa serikali katika kupunguza na vifo vya akina mama na watoto wachanga.

"Katika juhudi za kushughulikia changamoto za afya ya uzazi na akina mama, Serikali inaendelea kujenga wodi za wazazi kwa ajili ya akina mama wajawazito katika vituo vya afya nchini kote mijini na vijijini ili kutekeleza kampeni za afya ya uzazi. Hivyo ninapongeza Thamini

Uhai na wadau wengine wanaosaidia mpango huu na ninawaomba wananchi kutumia huduma hizi za afya. "Alisema.

Dr Paul Chaote, ambaye ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Kigoma, alisema kuwa ili kupunguza vifo vya uzazi, huduma mtambuka za dharura za uzazi zinapaswa kuwepo masaa ishirini nanne kwa siku saba za wiki (24/7).

Kwa hiyo, wanawake na familia zao wanapaswa kujua kwamba huduma zipo kwa kuwa na ufahamu wa faida zake na kutumia huduma za msingi, bila kuchelewa.

Kampeni itakuwa na matangazo ya redio na vipindi vya magazeti itatayojulikana kama“Mjamzito na Mtoto Salama ni Wajibu Wetu” ambavyo vitaruka hewani katika redio zifuatazo: redio Clouds. kupitia kipindi cha kila siku cha Leo Tena, Joy FM ya mjini Kigoma kila siku ya jumatatu, Jumanne, Alhamis na Jumamosi na redio Kwizera siku ya Jumatano, Ijumaa na Jumamosi. Kampeni pia itatumia vipeperushi, mabango, vibandiko, uhamasishaji jamii na mawasiliano ya kibinafsi ili kueneza ujumbe muhimu.

“Kampeni hii ina matumaini ya kuwafikia watu wengi mkoani Kigoma na kuwasaidia wanawake wajawazito na familia zao kuelewa vizuri haja ya kufahamu kuhusu afya ya uzazi na kupanga vizuri namna ya kujifungua. Hii itasaidia mkoa kuelekea kufikia malengo ya uzazi na watoto wachanga yaliyotajwa katika Mpango wa kitaifa wa afya (One Plan II) ", alisema Dk Nguke Mwakatundu, Mkurugenzi Mtendaji wa Thamini Uhai.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)