Pages

NAIBU WAZIRI DK. NDUGULILE AZINDUA BARAZA LA WATOTO MKOA WA SHINYANGA,AKABIDHI OFISI,KOMPYUTA

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile leo Jumatatu Februari 19,2018 amezindua Baraza la Watoto Mkoa wa Shinyanga na kukabidhi rasmi ofisi na kompyuta kwa ajili ya baraza hilo. 


Baraza hilo lenye wajumbe 12 likiwa na mwenyekiti,makamu mwenyekiti,katibu na mweka hazina na wajumbe sita mmoja kutoka kila halmashauri na watoto wawili wanaowakilisha watoto wenye ulemavu. 

Akizungumza wakati wa kuzindua baraza hilo, mjini Shinyanga, Dk. Ndugulile aliupongeza uongozi wa mkoa wa Shinyanga na kuutaka kuendelea kulea baraza hilo na mikoa mingine kuanzisha mabaraza ya watoto. 

“Wizara inaunga mkono kuanzishwa kwa baraza hili na tumetoa kompyuta moja itakayotumika kwa kazi za baraza,tunapenda kuona haki za watoto zinalindwa na ni wajibu wa kila mmoja kuwalinda watoto ili kuhakikisha haki zao hazivunjwi”,alieleza. 

“Naomba wajumbe wa baraza hili muwe mabalozi wa watoto wengine,heshimuni wazazi na walezi,nendeni shule na mjijenge katika maadili na tabia njema,msikae kimya, mpoona haki zenu zinavunjwa toeni taarifa,serikali ipo tuna sheria za kuwalinda”,aliongeza Dk. Ndugulile. 

Akisoma taarifa kuhusu kupatikana kwa baraza ,Mwenyekiti wa Baraza la watoto mkoa wa Shinyanga Victoria Chacha, alilishukuru shirika la Kimataifa la Save The Children kusaidia kwa kiasi kikubwa kuanzishwa kwa baraza ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa samani za ofisi ya baraza.  

Aliwataja wadau wengine waliofanikisha kuanzishwa kwa baraza hilo kuwa ni shirika la Rafiki SDO,AGAPE,ICS,Femina Hip na Redcross ambao wamekuwa wakishirikiana kwa ukaribu na maafisa maendeleo ya jamii. 

Mwenyekiti huyo alisema mbali na baraza hilo kufanikiwa kufichua matukio mbalimbali ya ukatili dhidi ya watoto bado matatizo ya ndoa na mimba za utotoni yanazidi kujitokeza ikiwa ni pamoja na ongezeko la vitendo vya ukatili na wimbi la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi. 

Aidha alimshukuru rais John Pombe Magufuli kwa kutangaza na kutekeleza sera ya elimu bure kuanzia darasa la saba hadi kidato cha nne kwani sera hiyo imekuwa mkombozi kwa watoto wengi.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile akizungumza wakati wa kuzindua Baraza la Watoto mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Februari 19,2018 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.Kushoto ni ni Kamishina wa Ustawi wa Jamii Dk. Naftali Ngo'ndi ,kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Wawakilishi wa watoto wanaounda baraza la watoto mkoa wa Shinyanga wakimsilikiza Dk. Faustine Ndugulile.
Dk. Faustine Ndugulile akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza la watoto mkoa wa Shinyanga.Wa kwanza kulia aliyeinama ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Rashid Mfaume.
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto mkoa wa Shinyanga, Victoria Chacha akisoma taarifa kuhusu Baraza la watoto mkoa wa Shinyanga . Alisema wamefanikiwa kupata chumba kwa ajili ya ofisi ya baraza la watoto mkoa na kupata misaada mbalimbali ikiwemo vifaa vya ofisi hiyo kutoka shirika la Save The Children na AGAPE.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile akishikana mkono na mwenyekiti wa baraza la watoto mkoa wa Shinyanga Victoria Chacha wakati wa kukabidhi mpango kazi wa Baraza la watoto mkoa wa Shinyanga kuanzia Januari 2018 hadi Disemba 2018.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile akikabidhi Mpango kazi wa Baraza la watoto mkoa wa Shinyanga kuanzia Januari 2018 hadi Disemba 2018 kwa mwenyekiti wa baraza hilo Victoria Chacha (kulia) na Makamu mwenyekiti wa baraza hilo Antonio Alfred (katikati).
Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile akikata utepe ishara ya kuzindua ofisi ya Baraza la Watoto mkoa wa Shinyanga mjini Shinyanga.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile akifungua mlango wa ofisi ya Baraza la Watoto mkoa wa Shinyanga. Ofisi ipo katika moja ya majengo yanayomilikiwa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Baraza la Watoto mkoa wa Shinyanga.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile akishikana mkono na Mwenyekiti wa Baraza la Watoto mkoa wa Shinyanga, Victoria Chacha wakati akikabidhi Kompyuta moja iliyotolewa na wizara anayoitumikia kwa ajili ya ofisi ya Baraza la Watoto mkoa wa Shinyanga.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile akikabidhi machapisho ya sheria ya mtoto na machapisho mengine yanayohusu haki na wajibu wa mtoto kwa viongozi wa Baraza la Watoto mkoa wa Shinyanga. Viongozi wa baraza wamepatikana kwa kupigiwa kura na wajumbe kutoka halmashauri zote sita za wilaya mkoa.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile akipanda mti nje ya ofisi ya Baraza la Watoto mkoa wa Shinyanga.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile akipiga picha ya pamoja na wawakilishi wa watoto wa baraza la watoto mkoa wa Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)