Pages

NAIBU GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA (BOT) AFUNGUA SEMINA YA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UCHUMI NA FEDHA MKOANI MTWARA

ki01
Bw. Julian Raphael Banzi Naibu Gavana wa Benki Kuu Utawala na Udhibiti wa Ndani (AIC) akifungua semina ya siku tano ya waandishi wa habari kuhusu masuala ya Uchumi inayofanyika katika ukumbi wa BOT Mtwara., Waandishi wa habari watapata ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu masuala ya uchumi, Kama vile Mabadiliko ya Mfumo mpya wa Kuandaa sera ya Fedha, Mapitio ya Maendeleo ya Uchumi nchini, Kikanda na Kimataifa BDuniani, Mifuko ya Dhamana kwa wajasiliamali na mengine mengi.
Akizungumza katika semina hiyo wakati akifungua semina hiyo amewashukuru waandishi wa habari kwa kazi kubwa wanayofanya katika kuandika habari za Benki Kuu kuhusu masuala ya uchumi, na pia akawaasa kuandika habari zinazohusu utekelezaji wa miradi mikubwa mbalimbali inayoendelea nchini kama ikiwemo Reli ya Kisasa (SGR), Miradi ya Umeme , Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda Mpaka Tanga nchini Tanzania na mingine mingi inayoendelea kutekelezwa.
ki5
Bw. Lucas Mwimo Mkurugenzi wa BOT Tawi la Mtwara akimkaribisha Bw. Julian Raphael Banzi Naibu Gavana wa Benki Kuu Utawala na Udhibiti wa Ndani (AIC) ili kufungua semina hiyo.
ki1
Bi Zalia Mbeo Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki (BOT) akitambulisha wageni mbalimbali katika semina hiyo.
ki3
Bw. Julian Raphael Banzi Naibu Gavana wa Benki Kuu Utawala na Udhibiti wa Ndani (AIC) kulia, Bw. Lucas Mwimo Mkurugenzi wa BOT Tawi la Mtwara katikati na Jonson Myella Mkurugenzi Tafiti za Uchumi (BOT) wakiwa katika semina hiyo.
ki6
Bw. Julian Raphael Banzi Naibu Gavana wa Benki Kuu Utawala na Udhibiti wa Ndani (AIC) na Bi Zalia Mbeo Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki (BOT) wakifuatilia hotuba ya Bw. Lucas Mwimo Mkurugenzi wa BOT Tawi la Mtwara hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa semina hiyo.
13
Jonson Myella Mkurugenzi Tafiti za Uchumi (BOT) na maofisa wenzake wakiwa katika semina hiyo.
ki7
Vick Msima Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki akiwa pamoja na maofisa wenzake kutoka BOT wakifuatilia hutoba ya Bw. Julian Raphael Banzi Naibu Gavana wa Benki Kuu Utawala na Udhibiti wa Ndani (AIC).
4
Vick Msima Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki akitoa ratiba kwa washiriki wa semina hiyo.
5 6 7
Mwenyekiti wa Semina hiyo Bw. Ezekiel Kamwaga akitoa maelezo mafupi kabla ya kuanza kwa semina hiyo.
8
Katibu wa Semina hiyo Dorcas Mtenga kutoka Chanel Ten akizungumza machache kabla ya kuanza kwa semina hiyo.
10
Mwenyekiti wa Semina hiyo Bw. Ezekiel Kamwaga akitoa maelezo mafupi kabla ya kuanza kwa semina hiyo.
12
Bw. Casmir Ndambalilo kutoka Idara ya Habari Maelezo akitaka ufafanuzi wa jambo katika semina hiyo kulia ni Goodluck Msola kutoka EFM.
ki2
Bw. Khalfan Said wa K-Vis Blog akifanya vitu vyake kwa ajili ya matukio ya semina hiyo.
IMG_1358
Bw. Julian Raphael Banzi Naibu Gavana wa Benki Kuu Utawala na Udhibiti wa Ndani (AIC) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina hiyo mara baada ya kufanya ufunguzi rasmi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)