Pages

Kibatala Kumtetea Sugu Baada ya Mawakili wa Mwanzo Kujitoa


Baada ya Wakili Boniface Mwabukusi na Sabina Yongo kujitoa kuwa wakili katika kesi inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Mbeya, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ inayoendelea kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya. Hatimae Wakili Peter Kibatala amechukua nafasi hiyo.

Sugu anakabiliwa na kesi ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Rais Magufuli. Ambayo wanadaiwa kuitoa Disemba 30 kwenye mkutano wa hadahara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mwenge. 

Katika mwendelezo wa kesi hiyo kumetokea mabishano yaliyopelekea Mahakama kuahirishwa kwa muda baada ya Wakili wa utetezi, Peter Kibatala kutaka aitwe mkuu wa upelelezi Mkoa wa Mbeya kama shahidi wao huku upande wa Jamhuri ukipinga kwa madai kuwa washtakiwa wanatakiwa kujitetea kabla ya shahidi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)