Pages

KATIBU MKUU UVUVI ATEKETEZA NYAVU HARAMU ZA BILIONI 2.6 MWANZA

Shehena ya nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa jina la operesheni Sangara zikiteketezwa kwa moto,Picha na John Mapepele
Shehena ya nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa jina la operesheni Sangara zikiteketezwa kwa moto,Picha na John Mapepele

Mkuu

wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha akishiriki kwenye zoezi la kuteketeza

nyavu haramu za uvuvi  zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6
zilizokamatwa
katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu
kilichoundwa
na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu
kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa
jina la operesheni Sangara zikiteketezwa kwa moto kulia mwenye suti ni
Katibu Mkuu wa Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia
Sekta ya Uvuvi, Dkt. Yohana 
Budeba akishuhudia,Picha na John Mapepele

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Yohana Budeba wa kwanza kulia aliyevaa suti akishirikiana na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana,Mary Tesha zoezi la kuteketeza nyavu haramu za uvuvi  zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa
katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa jina la operesheni Sangara
,Picha na John Mapepele

Na John Mapepele, Mwanza.


Katibu Mkuu wa Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Yohana Budeba ametaifisha na kuteketeza zaidi ya tani mia mbili za shehena ya nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa jina la operesheni Sangara .

Mbali na kuteketeza zana hizo haramu, Serikali pia imekusanya zaidi ya shilingi bilioni tano kama sehemu ya adhabu  kwa wavuvi na wafanyabiashara waliokutwa na zana haramu pamoja na makosa ya utoroshaji mwani, samaki na mazao yake nje ya nchi.

Akizungumza na mamia ya wavuvi wakati wa kuteketeza nyavu hizo leo, katika dampo la Buhongwa nje kidogo ya jiji la Mwanza, Dkt. Budeba amesema hatua hizo kali zinazochukuliwa na Serikali dhidi ya uvuvi haramu hazilengi kuwaonea wafanyabiashara au wavuvi wanyonge bali zimelenga kuwatengenezea maisha bora ya kizazi cha sasa na baadae ili kiweze kunufaika na rasilimali zilizoko ziwani.

Aidha Dkt. Budeba amesisitiza kuwa kikosi hicho kitaendelea na operesheni
hiyo bila kuchoka hadi hapo uvuvi haramu na utoroshaji wa mazao ya uvuvi
utakapokwisha ndani ya ziwa hilo.

Pia aliwaonya wamiliki wa  viwanda na wafanyabiashara wanaotengeneza
na kuuza nyavu hizo ambapo amesema Serikali ikiwabaini itawachukulia
hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na  kuwafutia leseni zote
za biashara zao.

Alisema rasilimali  zilizopo ndani ya ziwa hili ni mali ya wananchi
viongozi wamepewa dhamana ya kuongoza kazi ya ulinzi tu na endapo uvuvi
haramu utakomeshwa wananchi ndiyo watakaonufaika.

Pamoja na kuteketeza nyavu hizo haramu, Dkt Budeba alieleza hali ya upatikanaji wa samaki aina ya sangara katika Ziwa Victoria ambapo alisema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) mwaka 2017 unaonesha kuwa samaki waliochini ya sentimita 50 ni asilimia 96.6  hivyo samaki hawa ni wachanga na hawarusiwi kuvuliwa ambapo samaki walio zaidi ya sentimita 85 ni asilimia 0.4 tu ambao ni wazazi na hawarusiwi kuvuliwa pia. Samaki wa sentimita 50 mpaka 85 ambao ndio wanafaa kuvuliwa ni asilimia 3 tu.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi wa Wizara ya Mifugo
na Uvuvi, Fatma Sobo amesema Idara itaendelea kutumia Sheria ya Uvuvi
namba 22 ya mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2009 pamoja na Sheria
nyingine za Mazingira ili kudhibiti Uvuvi haramu nchini.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha alisema Serikali ya Wilaya
hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za kupambana na uvuvi haramu na
kuwachukulia hatua stahiki kuwataka wananchi kuendelea kuwafichua wavuvi haramu ili kulinda rasimali  hiyo muhimu waliyopewa na
Mungu.

Kwa upande wao baadhi ya wavuvi walimuomba Dkt. Budeba kuwasiliana na Wizara ya Viwanda na Biashara, ili kuona namna ya kudhibiti nyavu zisizoruhusiwa ambazo zinatengenezwa viwandani na baadae kuuziwa wavuvi.

Hivi karibuni watendaji wakuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana  na kikosi kazi kilichoundwa na Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi  wameweza kukamata  nyavu haramu, meli za uvuvi kutoka nje ya nchi zinazovua bia kufuata taratibu na mazao ya uvuvi yanayotoroshwa nje ya nchi ikiwemo mwani na samaki yenye mabilioni ya fedha huku Waziri Mwenye dhamana ya sekta hiyo Luhaga Mpina kuahidi kuwa  operesheni hizo zitakuwa za kudumu hadi uuvi haramu utakapokoma.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)