Pages

DC GONDWE AWAFUNDA VIJANA VIBAONI FC IKITWAA UBINGWA WA UCHUMI CU 2017-2018

 Mbunge wa Handeni, Omary Kigoda (kushoto) akimkabidhi zawadi ya mipira, Nahodha wa timu ya Kurugenzi Fc, Nguluko Machele, baada ya timu yake kuibuka mshindi wa pili katika michuano ya UCHUMI Cup iliyomalizika jana jumapili katika Uwanja wa CCM Kigoda mji wa Handeni Mkoani Tanga. Michuano hiyo iliandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe (katikati) kwa lengo la kuwahamasisha vijana kujihusisha na Kilimo cha Mihogo na mazao mengine ili kukuza uchumi wa wilaya hiyo. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
*****************************************
Na Muhidin Sufiani, Handeni
VIJANA wametakiwa kujitambua kukuza vipaji vyao walivyonavyo ili waweze kufika mbali na kuweza kujenga uchumi wa nchi kupitia vipaji.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe, wakati akizungumza katika hafla ya kuhitimisha mashindano ya UCHUMI Cup yaaliyomalizika katika Uwanja wa CCM Kigoda uliopo mji wa Handeni Mkoani Tanga,jana.
Alisema kuwa baada ya mashindano hayo ni mwanzo wa Msimu wa Kilimo na Uelewa wa Vijana kuhusu suala zima la Kilimo cha mihogo ili kuunga mkono kauli ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli ya HAPA KAZI TU na Uchumi wa Viwanda kupitia kilimo.
Aidha alitaka vijana kujitahidi kuwa wawazi katika kutambua na kuweka wazi vipaji vyao ambapo alisema kuwa baada ya kumalizika michuano hiyo na kutambua kuwa mji wa Handeni una vijana wenye vipaji sasa michuano hiyo itakuwa ni endelevu na ili kuhakikisha vijana wanapata nafasi ya kutoka na kucheza soka katika timu kubwa za ligi kuu.
Kwa kuonyesha jitihada hizo Kamati iliyokuwa ikiratibu mashindano hayo kwa kushirikiana na Viongozi wa Chama cha soka Wilayani hapo wamechagua wachezaji nyota kutoka katika kila timu,watakaounda kikosi cha timu ya Wilaya ya Handeni,ambayo itapata fulsa ya kucheza na moja ya timu kubwa ya Ligi kuu ambayo itatangazwa baadaye itakayokuwa tayari kwa ajili ya kuchagua vijana wenye vipaji.
Wakizungumza kwanyakati tofauti wadau mbalimbali wa soka wa Handeni,wamesema kuwa wanamshukuru sana Mhe. Dc Gongwe kwa kuwainua vijana wao katika suala zima la michezo na kusema kuwa michuano kama hiyo sasa imepita miaka 20 na zaidi katika mji huobila kuwa na mashindano ya aina yeyote yanayoleta hamasa kwa vijana.
Aidha wadau hao wamesema kuwa mara ya mwisho mashindano kama hayo yaliwahi kufanywa na aliyewahi kuwa Mbunge wa Handeni Marehemu Dkt.Omary Kigoda, ambapo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza na mwisho kuiona timu ya Simba ikicheza mchezo wa kirafiki katika uwanja huo wa CCM Kigoda.
''Hapa kwa mara ya mwisho kuwa na burudani kama hii ya leo na kushuhudia vijana wetu wakicheza kwa hamasa kubwa katika uwanja huu ilikuwa ni miaka 20 iliyopita ambapo pia tuliwaona Simba enzi hizo kina Julio bado vijana wadogo kabisa wakicheza hapa,lakini tangu hapo hapajawahi kutokea burudan kama hii ya leo,
Kwakweli tunamshukuru sana Mhe. Dc Gondwe kwa ubunifu wake na kuona kuna umuhimu wa kuwainua vijana katika michezo na kujitambua katika Kilimo kwani tuna ardhi nzuri na yenye rutuba ya kutosha wilayani kwetu inayokubari mazao''. alisema mdau wa Soka aliyejitambulisha kwa jina la Esau Ngadala, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa miguu Wilaya ya Handeni.
 Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Handeni,Asha Kigoda, akimkabidhi zawadi ya Jezi na mipira Kocha wa timu ya Netiboli ya Shule ya Sekondari Kivesa,Shani Salumu,baada ya timu yake kuibuka mshindi wa pili katika michuano ya UCHUMI Cup iliyomalizika jana katika Uwanja wa CCM Kigoda mji wa Handeni Mkoani Tanga. Michuano hiyo iliandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe (katikati) kwa lengo la kuwahamasisha vijana kujihusisha na Kilimo cha Mihogo na mazaomengine ili kukuza uchumi wa wilaya hiyo.
 Wachezaji wa timu ya Vibaoni wakishangilia baada ya kukabidhiwa medali zao na Kikombe kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa fainali hizo dhidi ya Kurugenzi.
 Mkurugenzi wa handeni, William Kufwe, akimkabidhi zawadi ya mipira na jezi Nahodha wa timu ya Netiboli ya Wanawake Live, Shani Salum, baada ya kuibuka washindi wa kwanza katika mchezo wa fainali za UCHUMI Cup dhidi ya Kivesa Sekondari. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya handeni, Godwin Gondwe.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa miguu Wilaya ya Handeni, Esau Ngadala, akimkabidhi Tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya UCHUMI Cup, Nahodha wa timu ya Kurugenzi, Nguluko Machele, wakati wahafla ya kukabidhi zawadi kwa timu zilizofanya vizuri katika michuano hiyoiliyomalizika jana katika Uwanja wa CCM Kigoda mji wa Handeni Mkoani Tanga. (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe. 
 Nahodha wa timu ya Kurugenzi, Nguluko Machele (katikati) akijaribu kuwatoka mabeki wa Vibaoni, Yusuph Ngole (kulia) na Jumanne Kisuse, wakati wa mchezo wa fainali za michuano ya UCHUMI Cup, iliyomalizika jana kwenye Uwanja wa CCM Kigoda Handeni mkoani Tanga, michuano hiyo iliandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe kwa lengo la kuhamasisha Vijana kujihusisha na Kilimo cha Mihogo na mazao mengine. Katika mchezo huo timu ya Vibaoni ilishinda mabao 3-0 na kutwaa kombe hilo la Uchumi Cup 2017-2018. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


 Mshambuliaji wa timu ya Kurugenzi Fc, Ernest Pindu (kulia) akichuana kuwania mpira na beki wa Vibaoni Fc, Mberwa Samuel, wakati wa mchezo wa fainali za michuano ya UCHUMI Cup, iliyomalizika jana kwenye Uwanja wa CCM Kigoda Handeni mkoani Tanga, michuano hiyo iliandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe kwa lengo la kuhamasisha Vijana kujihusisha na Kilimo cha Mihogo na mazao mengine. Katika mchezo huo timu ya Vibaoni ilishinda mabao 3-0 na kutwaa kombe hilo la Uchumi Cup 2017-2018. 
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe (kushoto) akizungumza jambo na Kocha wa Coastal Union, Juma Mgunda.....
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Handeni, Mgaya Ally Twaha, akimkabidhi zawadi ya Jezi, Nahodha wa timu ya Mtazamo Fc ya Mkata, Athuman Madanga, baada ya timu yake kuibuka mshindi wa tatu katika michuano hiyo. 
 Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Handeni, Thomas Mzinga, akiwavisha medali wachezaji wa Vibaoni Fc washindi wa michuano hiyo.
 Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Handeni, Thomas Mzinga, akimkabidhi zawadi ya Jezi Nahodha wa timu ya Vibaoni Fc, Omary Nyambwiro, ambao ni mabingwa wa michuano hiyo wa mwaka 2017-2018.
 Vibaoni wakishangilia......
 Raha ya ushindi kombe........
 Hapa mtanange wa kukata na shoka ukiendelea........
 Hii siyo Kung Fu bali ni soka la kiume hapa katika Uwanja wa CCM Kigoda Handeni Tanga
 Meza kuu wakifuatilia mtanange huo.....
 Timu zikisubiri kukaguliwa
 Mkuu wa Wilaya na baadhi ya viongozi wakikagua timu
 Meza kuu wakifuatilia mtanange
 Ulinzi pia ulikuwa ni wa kutosha kila kona
 Viongozi wakifuatilia mtanange huo kwa umakini
 Kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali kulikuwa na mchezo wa utangulizi kati ya timu ya Viongozi wa Chama na Serikali na Wafanyabiashara wa Mji wa Handeni. Katika mchezo huo Viongozi wa Chama na Serikali walishinda kwa mikwaju ya penati
 Kiungo mshambuliaji wa timu ya Chama na Serikali, Justice Mayela, akiambaa na mpira.
 Kiungo wa timu ya Wafanyabiashara, Mehebub Ismail, akiambaa na mpira....
 Daud Lugoya wa Chama na Serikali (kushoto) akiwania mpira na Mehebub Ismail wakati wa mchezo huo...
 Keilan Hussein 'Abai Chips' akiwatoka wachezaji wa Chama na serikali....
 Mbunge wa Handeni, Omari Kigoda akimchambua kipa wa wanyabiashara kwa mkwaju wa penati
 Mbunge wa Handeni, Omari Kigoda, akikimbia kwa madaha baada ya bao lake la penati
 Viongozi wakishangilia ushindi wa timu yao 
 Mhe. Dc akiwapongeza wachezaji wake.....
 Dc Gondwe akipiga picha na baadhi ya wachezaji wa timu ya Wafanyabiashara
 Dc Gondwe akizungumza na mganga wa timu ya Wafanyabiashara
 Dc Gondwe akipozi kwa picha na Juma Mgunda na Mbwiga Mbwiguke
 Huu ulikuwa ni mchezo wa fainali wa Netiboli kati ya Wanawake Live na Kivesa Sekondari. Katika mchezo huu Wanawake Live walishinda na kuwa mabingwa wa michuano hiyo 2017-2918
 Wasanii wa Vichekesho, Dkt. Nyau na mwenzake Kinyambi pia walikuwepo kuwakilisha.
 Wachezaji wa timu za Netiboli za Segera na Kabuku wakichuana wakati wa mchezo wa fainali za UCHUMI Cup kutafuta mshindi wa tatu, zilizomalizika jana katikaUwanja wa CCM KIgoda mji wa Handeni Mkoani Tanga.Michuano hiyo iliandaliwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Godwin Gondwe kwa lengo la kuwahamasisha vijana kujihusisha na kilimo cha Mihogo na Mazaomengine. Katika mchezo huo Segera walishinda mabao 26-13.
 Huu ulikuwa ni mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu kati ya Segera na Kabuku ambapo Segera waliibuka washindi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)