Pages

AWESO AHAIDI NEEMA KWA WAKANDARASI WA MAJI WAAMINIFU

Na Mwandishi Wetu.

Naibu Waziri wa Maji na Umwangiliaji, Mheshimiwa Jumaa Aweso ameahidi serikali kupitia wizara ya Maji kulipa kwa wakati wakandarasi waaminifu wanaosimamia miradi ya Maji ili upatikanaji wa Maji uwe endelevu.

Mheshimiwa Aweso ameyasema hayo Jijini Dar kwenye siku yake ya nne ya kikazi alipokuwa akikagua maendeleo ya miradi ya Maji inayotekelezwa na Manispaa pamoja na Miradi ya DAWASCO na DAWASA.

"Wizara ya Maji inajitahidi kutengeneza miradi ya maji itakayomaliza tatizo la Maji kwa wananchi hususani wananchi wenye kipato cha chini hasa vijijini, hivyo mkandarasi atakayefanya kazi yake vizuri na kwa wakati sisi kama serikali hatutasita kumlipa kazi yake kwa wakati"alisema Aweso

Katika ziara yake hiyo, Mheshimiwa Aweso alitembela miradi ya Maji ya Hondogo, Kibamba, Kingazi A pamoja na Mburahati.
Naibu Waziri wa Maji na Umwangiliaji, Mheshimiwa Jumaa Aweso akiangalia bomba lililopasuka.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)