Pages

WATOTO YATIMA 150 WAPATIWA MSADA WA VIFAA VYA SHULE

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe akiwaasa watoto yatima wa kituo cha Bethel Wilayani Gairo. Kulia kwake ni baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama walioambatana naye.
Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo Gairo, Mhe. Andrea Sendeha akitoa salamu kwa watoto yatima.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe akigawa zawadi kwa watoto yatima wa kituo cha Bethel kilichopo wilayani humo.
Watoto wa kituo cha Bethel Wilayani Gairo wakiwa wamejipanga mstari kupokea zawadi.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye nguo ya njano), Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo Gairo, Mhe. Andrea Sendeha (wa tatu toka kulia) pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wa kituo cha Bethel wa Gairo.

Na Mwandishi Wetu.

Katika kujali makundi yenye changamoto za maisha hasa watoto wadogo, Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe amegawa sare za shule na madaftari kwa watoto yatima 150 kituo cha Bethel Wilayani Gairo kinachosimamiwa na Mchungaji Chacha.

Hafla hiyo ya ugawaji wa vifaa ulifanyika mapema wiki hii, ambapo Mhe. Mchembe amesema kuwa huo ni utamaduni aliojiwekea kila mwanzo wa mwaka wa kuwakumbuka watoto yatima na wale waishi katika mazingira magumu.

"Nawakumbusha wananchi kujenga utamaduni wa kusaidiana watu wasiojiweza ili muweze kupata baraka kutoka kwa mwenyezi Mungu, unajua unapokuwa nacho ukatoa kidogo unabarikiwa zaidi," alisema Mhe. Mchembe.

Mhe. Mchembe aliwakumbusha watoto hao kuzingatia masomo kwani Serikali ya awamu ya tano ya Dr. John Magufuli inatoa elimu bure hivyo hakuna mtoto wa masikini atakayeshindwa kusoma.

Katika kukua kwao wamtangulize Mungu naye ataendelea kuwabariki na kuwatoa katika hali ya kuhisi unyonge wa kukosa wazazi.

Mwisho aliwaasa waalimu kuwa na moyo wa upendo kwa watoto yatima. Pia kuweka karibu hasa watoto wa kike kuwaepusha na mimba za utotoni.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)