Pages

WATOTO WANAOELELEWA VITUONI WAASWA KUJITAMBUA

WATOTO wanaolelelewa katika vituo vya kulea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi wametakiwa kujitambua na kujikubali ili kutekeleza wajibu wao wa kupokea malezi mema.

Aidha imeelezwa kuwa watoto wanathaminika sana ndio maana wapo watu wameamua kujitolea kuhakikisha wanaishi maisha ya kawaida na kuwa watu muhimu katika jamii.

Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam, wakati akizungumza na watoto wa wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis hivi karibuni. akimkabidhi Mama mlezi wa kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam, Getrude Nyalubamba (kushoto) akiwa ameongozana na Mwenyekiti kamati ya Msamaria mwema ya kanisa la Ukombozi, Leonard Masano (kulia) walipowasili kituoni hapo kwa ajili ya kukabidhi misaada mbalimbali.

Mchungaji huyo na kundi la wanawake na wanaume wa kanisa hilo walifika kituoni hapo kutembelea watoto hao na kuwapa zawadi mbalimbali.

Alisema katika hafla hiyo kwamba watoto hao wanapojiamini, kujikubali na kujithamini wataona manufaa yake hasa kwa kukubali malezi na kutambua uwepo wa walezi ambao wanajali maslahi yao.

Aidha alisema kwamba ni wajibu wa jamii na kanisa kwa ujumla kutekeleza kwa vitendo kujali yatima wajane na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi kwa kuwa kitendo hicho kina Baraka kubwa.
Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko (kulia) wa Kanisa la Ukombozi, akibeba gunia la unga kuingiza katika eneo la kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam hivi karibuni. Anayemsaidia ni mmoja wa wakazi wa kituo hicho Elizabeth Samweli anayesoma shule ya sekondari ya Pomerini, Iringa. Wanawake na wababa wa kanisa la Ukombozi walifika kituoni hapo wakiongozwa na mchungaji huyo kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali.

Alisema kwamba amefurahishwa kufika katika kituo hicho na kutekeleza wajibu wa kukaa pamoja na watoto hao na kumpongeza mama mlezi kwa kazi yake kubwa anayoifanya katika kuwahudumia watoto takribani 31 wanaoishi hapo.

Aliwataka watanzania kuwa na tabia ya kujali watoto hao kwa kuhakikisha wanapata mahitaji yao kila siku na sio siku ya sikukuu tu.

Kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilihamishwa kutoka Stop Over kwenda Mbezi Luishi ili kupisha matakwa ya sheria ya barabara ya Morogoro. Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wanaolelewa kwenye kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam wakisaidia kubeba zawadi mbalimbali zilizotolewa na kanisa hilo hivi karibuni.

Naye mmoja wa watoto 130 waliopita katika mikono ya kituo hicho tangu kianzishwe 1998, Oscar Gabone mwanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe aliwataka wananchi kufika kuwatembelea watoto hao na kuzungumza nao kuonesha upendo hata kama hawana kitu cha kuwapeleka.

Alisema kituo hicho kina changamoto nyingi hasa zinazotokana na kubomolewa kwa makazi yao Stop Over na kwamba juhudi za kujenga maboma ya wanawake na wavulana yanaendelea sio kwa kasi inayoridhisha.

Alitaka wananchi kuchangia ustawi wa watoto wa kituo hicho ambao wengi wamefikishwa wakiwa wadogo na wengine wakubwa kwa lengo la kuwapatia elimu na matunzo. Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi akizungumza na watoto yatima wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam alipotembelea kituo hicho hivi karibuni na kutoa misaada mbalimbali. Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam, Esther Pilila

Alisema kwamba sasa wana changamoto kubwa ya kuhamisha makao yao na hawana fedha na pia wanahitaji kujenga ghala la chakula.

Gabone alishawishi wananchi kuendelea kufika kituoni kuongea na watoto wa kituo hicho ili wawe na thamani ya upendo, si lazima wabebe kitu.

Mama Mlezi wa kituo hicho, Mama Getrude Nyalubamba alisema amefurahishwa na ziara hiyo ya kanisa, kwa kuwafikia na kuwapatia vitu mbalimbali kama nguo na vyakula katika kituo hicho na wakazi wake.
 
Mmoja kati ya watoto 130 waliopita katika mikono ya kituo hicho tangu kianzishwe 1998, Oscar Gabone mwanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe akifafanua jambo wakati walipotembelewa na waumini waliombatana na Mchungaji msaidizi Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi (hawapo pichani) hivi karibuni kituoni hapo.

Alisema kwamba anaamini Mungu anawapenda sana ndio maana watu wanafika kwao kuwaangalia.

Mmoja wa mabinti hao Rose Lemenga ambaye anasoma kidato cha 5 mkondo wa HKL shule ya sekondari Pomelin ameitaka jamii kuendelea kuwasaidia kutokana na wao kukabiliwa na changamoto nyingi za darasani na makuzi.

Kituo hicho kina watoto ambao wako shule ya msingi, sekondari na hata chuo kikuu.
Mama mlezi wa kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam, Getrude Nyalubamba akiwa amembeba mtoto Grace Tegete (1.5) aliyefika kituoni hapo baada ya mzazi wake kumtelekeza kwenye basi la abiria. Baadhi ya wasichana wanaolelewa kwenye kituo hicho wakimsikiliza Mchungaji msaidizi wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam, Faith Tetemeko (hayupo pichani) wakati alipotembelea kituo hicho kukabidhi misaada mbalimbali. Baadhi ya wanaukombozi na wageni wengine waliofika kituoni hapo kukabidhi misaada mbalimbali. Mwalimu Scolla (kushoto) wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam akibadilishana mawazo na baadhi ya wasichana wanaolelewa kwenye kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo jijini hapa. Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam, Esther Pilila na Mwenyekiti kamati ya Msamaria mwema ya kanisa hilo, Leonard Masano wakisaidiana kupanga misaada mbalimbali zikiwemo nguo na vyakula walivyokabidhi kituoni hapo hivi karibuni.
Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi, akimkabidhi Mama mlezi wa kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam, Getrude Nyalubamba moja ya bidhaa zilizowasilishwa hapo kwa ajili ya matumizi ya watoto wa kituo hicho. Anayeshuhudia ni Mwenyekiti kamati ya Msamaria mwema ya kanisa la Ukombozi, Leonard Masano. 
Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi akigawa zawadi ya juisi kwa mtoto Godfrey Steven anayeishi kituoni hapo wakati wa kukabidhi mahitaji mbalimbali kwa kituo hicho. Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi akiendelea na zoezi la ugawaji zawadi mbalimbali kwa kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam. Watoto wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luisi, Ubungo Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja na Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam, Esther Pilila katika hafla ya kukabidhiwa misaada mbalimbali iliyofanyika hivi karibuni kusherehekea mwaka mpya. Misaada hiyo ikiwamo chakula na mahitaji ya shule ilikabidhiwa kwa kituo hicho na kanisa la Ukombozi.
Mtoto Grace Tegete (1.5) anayelelewa kwenye kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam akifurahia ndani ya gari la mmoja wa wanaukombozi waliofika kituoni hapo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)