Pages

WAJASILIAMALI WATAKIWA KUTUMIA MAFUNZO YA SIDO KIKAMILIFU

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sporah Lyana akiongea na wajasiliamali mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akifunga mafunzo yaliyokuwa yameandaliwa na SIDO jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuwajengea uwezo na kuzipa thamani bidhaa wanazozitengeza. Pembeni yake ni Meneja wa SIDO Dar es Salaam, McDonald Maganga. Picha na Cathbert Kajuna -KAJUNASON/MMG.
Meneja wa SIDO Dar es Salaam, McDonald Maganga akitolea ufafanuzi mafunzo hayo ambayo wamekuwa wakiyatoa kwa wajasiliamali mbali mbali ili kuwajengea uwezo wa kuzipa thamani bidhaa zao wanazozitengeneza.


Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sporah Lyana (wa nne kutoka kushoto) na Meneja wa SIDO Dar es Salaam, McDonald Maganga anayemfuatia wakifurahia jambo na wajasiliamali mara baada ya kuhudhuria sherehe ya kufunga kwa mafunzo yao.
Wajasiliamali wakifurahia bidhaa walizozitenegeza wakati wa mafunzo.
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sporah Lyana akipata maelekezo ya bidhaa walizozitenegeza wakati wa mafunzo. 
Wajasiliamali wakipokea vyeti.
Wajasiliamali wakiwa katika picha ya pamoja.

Na Humphrey Shao.

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sporah Lyana amewataka wajasiliamali mkoa huo kuhakikisha kuwa wanayatumia vyema mafunzo waliyopata kutoka Shirika la Viwanda Vidogo nchini (SIDO).

Lyana amesema hayo jijini Dar es Salaam jana alipokuwa anafunga mafunzo ya siku tano kwa wajasiliamali yanayoendeshwa na Sido kwa ajili ya kuwawezesha wajasiliamali wadogo kuweza kusindika na kuongeza thamani bidhaa mbalimbali.

“sisi kama jiji tumeanda ampango kabambe wa utalii wa mkoa wa Dar es Salaam amabo utaweza kuwasaidia wajasiliamali wa ndani kuuza bidhaa zao hivyo kila mjasiliamali ahakikishe anajianda kwa kuandaa vitu vyaka katika ubora unaohitajika” amesema Lyana.

Aidha mkurugenzi huyo aliweka wazi kuwa kama wajasiliamali wote hao wataweza kufanya kama walivyofundishwa wataweza kumsaidia Rais juu ya kuipelekea nchini yetu katika uchumi wa kati ambao unategemea sana Viwanda hivyo kwa wao kila mmoja kama ataanzisha kiwanda kidogo kutaweza kupunguza tatizo la ajira katika baadahi ya maeneo.

Aliamaliza kwa kutoa wito kwa wadau na watu wengine kwenda kujifunza Sido hili iwe rahisi kurasimisha biashara zao ambazo walikuwa wanafanya kienyeji.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)